Gavana wa kijeshi DRC awaonya waasi hususan Maimai

Kivu Kaskazini, DRC

Gavana wa Kijeshi wa jimbo la Kivu kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, ameyaonya makundi ya waasi hasa ya Maimai kwamba hakuna mazungumuzo yoyote yatafanyika na kundi lolote la waasi kwa sasa. 

Luteni Jenerali Constant Ndima amesema katika kijiji cha Kichanga wilayani Maisisi, njia moja ya kuanza mazungumzo ni kusalimisha Silaha.

Gavana huyo wa kijeshi alikuwa anazungumza katika sherehe ambayo wapiganaji zaidi ya mia moja wamesalimisha silaha zao kwa hiari.

Hili ni tukio la hatua ya Gavana huyo ya kwanza tangu alipo tangazwa kuwa Mkuu wa Jimbo la Kivu kaskazini, katika juhudi za serikali ya Kinshasa kumaliza uasi unaoendelea upande huo wa taifa hilo.

Wananchi wa wilaya hiyo wameeleza matumaini ya kupatikana amani baada ya wapiganaji hao walokua wakishi huko kwa muda mrefu kusalimisha silaha zao.

Chanzo cha Habari : VOA Swahili