Upigaji kura uliyotarajiwa kufanyika katika muda wa siku 10 zijazo hautafanyika pia katika jimbo la Tigray ambako kuna mzozo unaoendelea kwa wakati huu.
Maafisa wa uchaguzi wanasema kasoro za upigaji kura na matatizo ya kuchapisha vyeti vya kura yamesababisha kucheleweshwa kufanyika uchaguzi huo.
Shirika la habari la Uingereza, Reuters limemnukuu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Birtukan Mideksa akisema kwamba katika baadhi ya wilaya uchaguzi utafanyika mnamo duru ya pili hapo Septemba 6.
Hakuna tarehe iliyotajwa kwa ajili ya uchaguzi wa Tigray. Uchaguzi mkuu ulipangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2020, lakini uliahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona.
Chanzo cha Habari : Reuters