Ukosoaji ulijitokeza ndani ya ukumbi wa Miami Florida wakati mgombea mwenza seneta wa California Kamala Haris alivyomkabili vikali Biden na kusema miongo minne iliyopita alipinga kuwepo mabasi ya kuwachukua wanafunzi ili kuziunganisha shule.
Harris alielezea maskitiko yake makubwa aliposikiliza matamshi ya Biden akikiri kuwa alipokuwa seneta kijana alishirikiana na maseneta wabaguzi kwa kupasisha mswada wa sheria ambao Harris aliutaja kama waubaguzi dhidi ya wamarekani weusi.
Harris ambaye ni mwendesha mashtaka wa zamani wa serikali alimgeukia Biden na kusema, “Siamini kuwa wewe ni mbaguzi.” Lakini seneta huyo Marekani mweusi aliwafurahisha waliohudhuria mdahalo huo katika ukumbi wa mikutano Miami, Florida aliposema “inaumiza kusikia” kile Biden hivi karibuni alichoeleza kama seneta kijana alifanya kazi na maseneta wabaguzi wa maeneo ya kusini kupitisha sheria za ubaguzi.
“Hiyo ni kunipa wasifu usiolingana na nafasi yangu katika jamii,” alijibu Biden aliyekuwa amekunja uso wake. “Mimi sikuwa nakubali vitendo vya ubaguzi.”
Lakini Harris alishinikiza katika shutuma hizo, akimtaka Biden kueleza, "Je, unakubali ilikuwa ni makosa kupinga matumizi ya basi za kuwapeleka wanafunzi shule zilizokuwa zinawaunganisha wanafunzi wa rangi zote?
Harris alisema alinufaika na mradi wa mabasi ya shule na kumwezesha kuhudhuria masomo katika shule zilizokuwa hazina ubaguzi.
Mwaka wa 1970, mahakama iliamua kwamba mswada huo wa sheria utenganishe Wamarekani katika miji mingi ya marekani.