Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:21

Obamacare: Nini hatma ya bima ya afya baada ya uamuzi wa mahakama Texas?


Kiongozi wa chama cha Demokrat katika Bunge la Marekani Nancy Pelosi
Kiongozi wa chama cha Demokrat katika Bunge la Marekani Nancy Pelosi

Wabunge wa chama cha Republikan wamekuwa kimya juu ya uamuzi uliotolewa na mahakama Ijumaa kuwa sheria ya bima ya afya, ijulikanayo kama Obamacare (ACA), inakwenda kinyume na katiba.

Hata hivyo Wademokrat wamesema watakiwajibisha chama cha Republikan kuheshimu ahadi zake kwa kuendelea kuweka vipengele vinavyohitajika sana katika sheria hiyo, kama vile kuwahakikishia watu wenye magonjwa wanaohitaji tiba wataweza kuendelea kupata matibabu hayo.

“Chama cha Republikan kilitumia mwaka mzima (2017) wakijionyesha kama kwamba wanataka kuwasaidia watu ambao tayari wanatibiwa kutokana na maradhi walio kuwa nayo kwa kuendelea kuwawezesha kupata matibabu na wakati huohuo walikuwa wanajaribu kuondoa huduma hiyo kwa siri kupitia mahakama mbalimbali,” Kiongozi wa Wademokrat katika Baraza la Seneti Chuck Schumer kutoka New York alisema katika ujumbe wa tweet Jumamosi. “Mwaka ujao tutalazimisha kupiga kura ili tudhihirishe uongo wao.”

Mwakilishi wa Marekani Nancy Pelosi, Mdemokrat kutoka California ambaye ataanza kushikilia nafasi ya spika wa Bunge la Marekani mwaka 2019, amesema Bunge “litaanza rasmi mara moja kuingilia mchakato wa rufaa mbalimbali ili tuweze kuwaokoa na kuwalinda watu wenye hali za maradhi yanayo hitaji matibabu na kupinga juhudi za Warepublikan za kuitokomeza sheria hiyo.

Jaji wa Wilaya wa Marekani Reed O’Connor huko Jimbo la Texas alitoa uamuzi Ijumaa kwamba mabadiliko ya sheria ya kodi ya mwaka 2017, iliyoondoa adhabu kwa kutokuwa na bima ya afya ilifuta sheria hiyo ya bima ya afya, ACA.

Uamuzi huo wa mahakama unatarajiwa kukatiwa rufaa katika Mahakama ya Juu ya Marekani, na sheria hiyo ya ACA itaendelea kutumika wakati rufaa hiyo inaendelea.

Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa ameahidi wakati wa kampeni yake ya urais kuipangua Sheria hiyo ya bima ya afya (ACA), progamu ambayo iliweka bima ya afya nchini iliyoweza kuwafikia mamilioni ya Wamarekani na kuwawezesha kupata matibabu.

XS
SM
MD
LG