Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:25

Trump: Bima ya afya kwa kila mtu iko njiani kukamilika


Rais mteule wa Marekani, Donald Trump. Januari 13, 2017.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump. Januari 13, 2017.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amesema mpango wake mbadala wa programu ya afya iliyoanzishwa na Obama “unatayarishwa hadi kipengele cha mwisho,” na utazinduliwa rasmi karibuni.

Katika mahojiano na gazeti la Washington Post Jumapili, Trump amesema lengo lake ni kuwa “kila mtu awe na bima,” lakini hakutoa maelezo zaidi.

Kitu kimoja ambacho amekianisha ni kule kutaka kwake kupunguza gharama za huduma za afya kwa kushinikiza kampuni za madawa kupunguza bei zake.

Kufuta sheria ya huhuma za afya inayojulikana kama Obamacare, ni moja ya vipaumbele vya Trump wakati atapakochukua rasmi madaraka. Sheria hiyo iliyopitishwa na bunge mwaka 2010 ilikuwa wakati wa Demokrat walipokuwa na wingi katika mabaraza yote mawili ya Seneti na Wawakilishi.

Hivi sasa kwa kuwa Trump ni rais wanaweza wa Republikan kuchukua hatua kufanya mabadiliko ya mfumo ambao wanadai ni wa gharama ya juu na haufanyi kazi.

Wiki iliyopita, Bunge lilipitisha hatua za mwanzo za kuifuta sheria ya afya, japokuwa wa Republikan hawajaweka wazi mpango mbadala wa program hiyo, ambayo iliwapatia bima ya afya zaidi ya wamarekani milioni 20.

Trump pia ameliambia gazeti la Post timu yake iko karibu kumaliza mpango ambao ameuita ni upunguzaji “bora” wa kodi kwa watu wenye kipato cha kati na utapunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 15 katika juhudi za kutengeneza nafasi zaidi za ajira.

Rais mteule pia alifanya mahojiano na gazeti la The Times la Uingereza na gazeti la Ujerumani la Bild akiwaambia kuwa Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel alifanya makosa kuwaruhusu maelfu ya wahamiaji kuingia Ujerumani mwaka jana.

Trump amesema, “ Nafikiri amefanya kosa lililoleta msiba mkubwa kwa kuwaruhusu hawa wavunja sheria, unajua, kuwachukua watu wote hawa popote walipotokea.”

Wengi ya wahamiaji ni waislamu ambao walimiminika kutoka Ulaya wakikimbia vita, ugaidi na umaskini katika maeneo ya Syria, Iraq na Afghanistan.

Trump aliharakisha kusema kuwa siku zote alikuwa anampa heshima kubwa Merkel na alikuwa anamchukulia ni Kiongozi mzuri. Lakini amesema Ujerumani “ilipata sura kamili” ya matokeo ya sera yake ya uhamiaji – akijaribu kurejea tukio la shambulizi la lori la Disemba kwenye soko la Krismasi lililouwa watu 12.

Dereva ambaye aliwagonga waliokuwa wanafanya manunuzi katika soko hilo ni raia wa Tunisia aliyeingia Ujerumani kabla ya Merkel kufungua milango kwa wakimbizi waliotokea Mashariki ya Kati. Alikimbilia Italy baada ya shambulizi hilo na baadaye aliuwawa na polisi.

Trump amelaumu mgogoro wa wakimbizi kama ni sababu ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya na kuliita “ni pigo lililo mvunja ngamia mgongo.”

“Naamini hivi ndivyo ilivyo. Kama Umoja wa Ulaya isingelazimishwa kuchukua wakimbizi wote, wengi… Nafikiri kuwa msingekuwa na Brexit.”

Lakini bado alisema Brexit ilikuwa kitu kizuri, na akatabiri kuwa nchi nyingine zitajitoa katika Umoja wa Ulaya, akisema wao, kama Uingereza, wanataka utaifa wao.

“Nafikiri kuwa na umoja halitokuwa jambo rahisi kama watu wanavyofikiria. Iwapo wakimbizi wataendelea kumiminika katika maeneo mbali mbali ya Ulaya… watu wanahasira juu ya hilo.”

Trump pia ameyaambia magazeti ya Uingereza na Ujerumani kuwa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Ulaya (NATO) “umepitwa na wakati” kwa sababu uliundwa miaka mingi iliyopita.. na nchi hazilipi kile wanachotakiwa kulipa… ni imepitiwa na wakati kwa sababu haikuwa wanashughulikia suala la ugaidi.

Lakini ia amesema kuwa NATO ni muhimu sana kwake.

XS
SM
MD
LG