Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:59

Warepublican wanatofautiana kuhusu kuifuta Obamacare


Seneta Ted Cruz kutoka Texas kwa chama cha Republican.
Seneta Ted Cruz kutoka Texas kwa chama cha Republican.

Maseneta wawili wa chama cha Republikan nchini Marekani wameelezea upinzani wao siku ya Jumapili juu ya mpango wa karibuni wa chama hicho wa kufuta sera za huduma nafuu za afya.

Sera hizo zilipitishwa na Rais wa zamani wa Marekani kutoka chama cha Democrat Barack Obama na hivyo kutia mashaka kwasababu kura muhimu ambazo zingeweza kufuta mpango huo sasa zinaweza kudumaza juhudi hiyo.

Seneta Susan Collins wa jimbo la Maine amekiambia kituo cha televisheni Marekani cha CNN kuwa anaona vigumu sana kufikiria kupiga kura kufuta mpango wa huduma nafuu za afya ambao maarufu kama Obamacare.

Pia amesema kwamba hayuko tayari kutangaza kwa uhakika kwamba atapiga kura dhidi ya kuufuta mpango huo.

Senata Susan Collins, mrepublican jimbo la Maine.
Senata Susan Collins, mrepublican jimbo la Maine.

Seneta Collins alisema anataka kusubiri tathmini ya pendekezo la ofisi huru ya bajeti katika bunge juu ya ripoti hiyo inayotarajiwa kutolewa Jumatatu.

Wakati huo huo Senetal Ted Cruz wa jimbo la Texas amesema haungi mkono mpango wa kufuta sheria hiyo kwasababu hadhani mabadiliko yanafanya vya kutosha kupunguza gharama za bima kwa wateja. Seneta Cruz amesema hivi sasa hawana kura yangu.

XS
SM
MD
LG