Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:21

Mbunge mpya Msomali-Mmarekani apigania kanuni za uhuru wa kuabudu


Ilhan Omar (D-MI) akiwasili ndani ya ukumbi wa Bunge la Marekani kama mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Washington, Jan. 3, 2019.
Ilhan Omar (D-MI) akiwasili ndani ya ukumbi wa Bunge la Marekani kama mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Washington, Jan. 3, 2019.

Ilhan Omar anabadilisha sura nzima ya Bunge la Marekani. Omar – moja wa wawakilishi wawili ambao watakuwa ni Waislam wa kwanza wanawake kutumikia Bunge la Marekani –Congress – wanavaa hijabu. Lakini chaguo lake la hijab kiutaratibu linazuiwa chini ya kanuni za Baraza la Wawakilishi wa Marekani.

Bunge la Congress la 116 litakuwa ni lenye mchanganyiko kupita yote yaliyopita. Wakati Wademokrat wakiwa ni walio wengi katika bunge hilo wiki hii, watakuwa wanabadilisha sheria hizo kulingana na hali halisi.

Kanuni ambayo ingemzuia Omar kuvaa hijab iliandaliwa miaka 181 iliyopita, wakati Bunge la Marekani – Congress ilikuwa ni pahali tofauti. Wanawake na makundi madogo hayakupata fursa kutumikia kama wawakilishi siku za nyuma.

Wakati wabunge wakiamua “kila mwakilishi lazima awe hajajifunika wakati mkutano wa bunge ukifanyika,” walikuwa wanakusudia utamaduni wa wanaume katika karne ya 19 wa kuvaa kofia.

Kanuni hii ilikuwa haijawekwa kwa ajili ya kuyabagua makundi madogo ya kidini.

Lakini hata wakati huo sheria hiyo ilileta utata. Baadhi ya wawakilishi walikuwa wanadai kuwa kuvaa kofia ilikuwa inakumbusha utamaduni muhimu wa Bunge la Uingereza uliokuwa ni ishara ya uhuru kutoka utawala wa kifalme.

Wengine wanahoji katika hali ya utaratibu wa kila siku, wapi wataziacha kofia zao.

Lakini kisheria – na kusisitiza kwake juu ya heshima ya utamaduni huo – lilikuwepo tangu zama hizo. Kofia ni moja tu ya vitu vingine vingi vilivyo katazwa ndani ya Bunge. Sigara, chakula na simu haziruhusiwi chini ya kanuni za Bunge.

XS
SM
MD
LG