Ameeleza kiwango cha dola trilioni 4 zitatumiwa na serikali katika miradi ya miundombinu, uchumi na kuboresha maisha ya mamillioni ya Wamarekani.
Katika hotuba yake, Biden amesema kwamba amerithi nchi ambayo ilikuwa katika mzozo kutokana na janga baya ambalo halijawahi kutokea kwa karne nzima.
Pia nchi ilikuwa inakabiliwa na mzozo mbaya wa kiuchumi tangu enzi za kudorora kwa uchumi na shambulio baya kwa democrasia ya Marekani tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Biden alitumia dakika 65 za hotuba yake kuelezea zaidi sera ya masuala ya ndani. Alipendekeza mpango wa dola trillioni 1.8 kuongeza msaada wa serekali kwa watoto na familia za wa marekani.
Amesema mpango wake wa matumzi makubwa kwa ajili ya miundo mbinu, uundaji wa ajira na elimu unaeleweka kwa sababu China na nchi nyingine zina maendeleo ya haraka kwa sababu ya kuwekeza kwenye miundo mbinu.