Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:57

Makamu rais na spika waweka historia katika hotuba ya rais bungeni


Rais Biden akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya siku 100 madarakani.
Rais Biden akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya siku 100 madarakani.

Rais Joe Biden ametoa hotuba yake ya kwanza ya kwanza wakati wa kikao cha pamoja cha Bunge Jumatano usiku, huku akiadhimisha siku 100 tangu aingie madarakani .

Wakati huo huo mamilioni ya wamarekani wakishuhudia historia ikiandikwa ya kuwapo wanawake wawili waandamizi ndani ya bunge kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo wakati wa hotuba ya kwanza ya rais.

Rais Biden alianza hotuba yake kwa kutambua hatua iliyopiga Marekani na yeye kupata fursa ya kuwa rais wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kufungua hotuba yake ya kwanza baada ya siku 100 akiwa na spika wa Baraza la wawakilishi mwanamke na kiongozi wa shughuli za bunge ambaye pia ni makamu rais mwanamke.

"Baada ya siku 100 za uokoaji na kujenga upya, Marekani iko tayari kusonga mbele” Rais Joe Biden alisema katika kikao cha pamoja cha Bunge, akitumia fursa hiyo pia kushinikiza mapendekezo yake ya dola trilioni 4 katika matumizi ya serikali na utendaji wake wote katika kukabiliana na mfululizo wa mizozo ya kihistoria tangu kuchukua madaraka mwezi Januari.

Hotuba hiyo imefanyika mbele maseneta na wabunge wachache ndani ya jengo hilo kutokana na vizuizi vya janga la Covid -19 . Mchambuzi wa siasa kutoka Chuo kikuu cha Maryland Salisbury Profesa Fulbert Namwamba amepokea hotuba hiyo ya rais Biden akisema “amegeuza jambo ambalo lilikuwa mgogoro kuwa fursa” akilenga kuimarisha familia za Marekani na kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu ambayo itatoa fursa kubwa ya ajira, huku akiongeza kwamba Marekani inasonga mbele baada ya kutoka kwenye shida ya ugonjwa wa covid 19.

Profesa Namwamba pia anasema kuwepo kwa viongozi wa juu wawili wanawake bungeni ni ishara ya Marekani kusonga mbele na anaona Biden ameeleza juu ya kuamka kwa Marekani na kupitia kwenye bonde la kiza kutokana na ugonjwa huu wa covid akigusia kazi aliyofanya ya kutoa chanjo zaidi ya milioni 200 katika siku zake 100 za kwanza madarakani huku akiwa amewekeza fedha kwenye uchumi akiashiria kwamba hiyo imeamsha Marekani.

XS
SM
MD
LG