Serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) inawalaumu wanajeshi wa Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa mashariki ya nchi hiyo, kwa mashambulizi ya roketi walioyafanya katika mji mkuu wa Tripoli Jumanne usiku.
Mashambulizi hayo yamefanyika wakati baraza la usalama la UN likiwa linajadili muswada wa kusitisha mapigano uliowasilishwa na Uingereza unaotaka usitishaji wa mapigano mara moja.
Wafanayakazi wa huduma za dharura wanasema watu wawili waliuawa na wengine 11 kujeruhiwa katika mashambulio mawili kwenye mitaa ya kusini mwa Tripoli.
Waandishi habari wa shirika la habari la AFP wanaripoti kuwa wamesikia milio ya roketi kadhaa katikati ya mji, wakisema ni mashambulizi ya kwanza tangu wanajeshi wa Haftar kuanza uvamizi wa mji huo April 4.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.