Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:59

Wahamiaji waelezea unyanyasaji Kuwait, Libya


Mariama Ndow aliyekuwa Kuwait
Mariama Ndow aliyekuwa Kuwait

Mariama Ndow ni mmoja wa mamia ya wahamiaji ambao wamerejea Sierra Leone mwaka 2018. Anafurahia uhuru wake baada ya kukaa kwa takriban miezi kumi nchini Kuwait.

Kwanza alidhani anakwenda kufanya kazi huko kama mlinzi. Alipofika huko aliuzwa kama mfanyakazi wa nyumbani kupitia wakala anayehudumia familia kadhaa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:37 0:00

Ndow anasema alilipwa mara moja tu katika muda wote aliokuwa huko. na alilazimishwa kufanya kazi kwa takriban saa 24 kwa siku. Alipougua kulikuwa hakuna wa kumuonea huruma.

Alifanikiwa kukimbia wakati familia aliyokuwa akiifanyia kazi ilipokuwa imetoka. Kwa msaada wa mtu asiyemfahamu kwenye mitaa ya Kuwait, alielekezwa kwenda ofisi ya kimataifa ya kuhudumia wahamiaji IOM.

Manyanyaso kwa wahamiaji yanatokea sehemu nyingi. Libya inashutumiwa kuwa wahamiaji wanauzwa katika masoko ya watumwa.

Takriban wahamiaji 60 walirejeshwa kwamba msaada wa IOM na serikali ya sierra leone katikati ya mwezi December na kundi jingine lilirudishwa mwishoni mwa mwezi November.

Umari Barrie ni mmoja wa wahamiaji ambaye amerejea hivi punde kutoka Libya. Aliondoka Sierra Leone kwa sababu alikuwa hana ajira wala hana makazi.

Wahamiaji wengi wanaitumia Libya kama njia ya kuelekea ulaya. Umoja wa mataifa unakadiria kuwa kiasi cha wahamiaji 700,000 wako nchini Libya. Lakini anasema alitaka kubakia nchini Libya lakini ghafla akabaini kuwa maisha huko nayo si mazuri hata kidogo.

Pia ameelezea kuwa si mara zote unalipwa kwa kazi unayofanya. Na mke wake, ambaye wamekutana nchini Libya, mara kwa mara alikuwa halipwi ujira wake.

Hatimaye alifanikiwa kuwasiliana na IOM nchini Libya na kuanza utaratibu wa kurejeshwa nchini Sierra Leone. Barrie, na mke wake na mtoto wake wa kiume waliwasili nyakati za alfajiri Desemba14 kwa ndege ya kukodisha. Ilikuwa ni furaha.

IOM pia itamlipa fidia Barrie na ana matumaini ya kuanzisha biashara. Kwa sasa, anaishi na kaka yake. Ingawaje mwanzo ni mgumu sana, lakini bado, ana shukuru kuondoka Libya na kurejea nchini kwake.

XS
SM
MD
LG