AU yatangaza kauli mbiu ya 'Nyamazisha Bunduki' barani Afrika

President of South Africa Cyril Ramaphosa speaks during a state funeral of Zimbabwe's longtime ruler Robert Mugabe, at the national sports stadium in Harare, Zimbabwe, Sept. 14, 2019.

Viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) wanaokutana mjini Addiss Ababa wamesisitiza watachukuwa jukumu muhimu zaidi katika kutanzua migogoro inayoendelea katika bara hilo.

Huu ni mkutano wa kawaida wa kikao cha 33 cha pamoja cha wakuu wa nchi na serikali ya Umoja wa Afrika wa siku mbili unaomalizika chini ya kauli mbiu Nyamazisha Bunduki barani Afrika.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat alizungumzia jinsi usalama ulivyozorota katika sehemu mbali mbali za bara hilo kutokana na kuongezeka kwa ugaidi, ugomvi kati ya jamii mbali mbali na mizozo baada ya uchaguzi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anayechukuwa uwenyekiti wa umoja huo kutoka kwa Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri, ametanganza kwamba anania ya kuitisha mkutano wa viongozi mwezi May kuzingatia juu ya namna ya kutanzua migogoro na utekelezaji wa mkataba wa biashara huru barani Afrika.

Viongozi wa Afrika wanasema watajihusisha zaidi na kwa nguvu katika kumaliza mizozo ya Libya na Sudan Kusini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres ametangaza kuongeza msaada kwa walinzi wa amani barani Afrika akisisitiza haja ya kumaliza migogoro na kuzingatia maendeleo ya kiuchumi na kupambana na ghasia za kijinsia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.