Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:21

AU : Mpango wa amani wa Trump unawakandamiza Wapalestina


 Moussa Faki Mahamat
Moussa Faki Mahamat

Viongozi wa Afrika wamelaani pendekezo la mpango wa amani Mashariki ya Kati ulitolewa na Rais Donald Trump wa Marekani, wakisema haufuati sheria, wakichukua fursa hiyo cha Kilele cha mkutano wa viongozi kutangaza mshikamano wao na “juhudi za Wapalestina”.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat, amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kawaida wa 33 wa kikao cha pamoja cha wakuu wa nchi na serikali ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa, Ethiopia, Jumapili.

Ameeleza kuwa mpango huo “unakandamiza haki za wananchi wa Palestina”- tamko lililopongezwa katika ukumbi huo wa AU nchini Ethiopia.

Mahamat, ambaye alitumia hotuba yake hiyo kurejea mshikamano wa Afrika na juhudi za Wapalestina, alisema mpango wa Trump uliandaliwa bila kushauriana na jumuiya ya kimataifa, na kwamba unazikandamiza haki za Wapalestina.

Wachambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati walieleza mpango huo uliopewa jina la makubaliano ya karne, ulikataliwa tangu mwanzoni na Wapalestina wakiungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na mataifa jirani ya Mashariki ya Kati, Ghuba na ulimwengu wa Kiislamu.

Pendekezo hilo la Trump liliochukuwa muda mrefu hadi kutangazwa mara moja lilikataliwa na Wapalestina, ambao wamegoma kushirikiana na uongozi wake kwa sababu ya madai yao ya kuwepo upendeleo kwa Waisraeli.

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina, ambaye kawaida huhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika kama mgeni mwalikwa, mara hii ameshindwa kuhudhuria, huku maafisa wa serikali yake wakisema anaelekea Umoja wa Mataifa kulishinikiza Baraza la Usalama kuulaani mpango huo wa amani.

XS
SM
MD
LG