Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:36

Mazishi ya Taifa : Kenyatta atoa wasifu wa pongezi kwa Rais Moi


Rais Kenyatta akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais Moi. Picha zote kwa hisani ya ikulu ya rais Kenya.
Rais Kenyatta akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais Moi. Picha zote kwa hisani ya ikulu ya rais Kenya.

Rais Uhuru Kenyatta Jumamosi ametoa wasifu wa pongezi kwa Rais wa zamani Daniel Toroitich arap Moi wakati akizundua shughuli za mazishi rasmi ya kiserikali kabla ya mwili wa Rais wa pili wa Kenya kwenda kuzikwa.

Kenyatta akiuaga mwili wa Rais wa zamani Moi
Kenyatta akiuaga mwili wa Rais wa zamani Moi

Rais Kenyatta ambaye aliwasili nchini akitokea Marekani usiku wa jana, alianza siku yake kwa kuongoza kikao kisicho cha kawaida cha mawaziri kilicho hudhuriwa na Naibu Rais William Ruto, Mawaziri na kamati ya mazishi yaliyoongozwa na Mkuu wa Huduma za Umma Joseph Kinyua, taarifa ya ikulu ya Kenya imeeleza.

Baraza la Mawaziri lilikutana kujadili maadalizi ya taifa kwa ajili ya hatua ya mwisho ya mazishi ya Rais wa zamani atakaye kumbukwa kwa kuhakikisha Kenya inabakia kuwa imara wakati wa machafuko yaliyokuwa yanaendelea katika bara la Afrika katika kipindi cha miaka 24 ya utawala wake.

Rais Kenyatta akiwasili katika maziko na kupokelewa na Makamu wake Ruto
Rais Kenyatta akiwasili katika maziko na kupokelewa na Makamu wake Ruto

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kikao cha mawaziri, Rais Kenyatta alimpongeza Mzee Moi kama “mtoto shupavu wa Kenya, ndugu mpendwa, baba mwenye upendo, mlezi wa wengi, na baba wa taifa letu na aliyeunga mkono umoja wa Afrika.

Rais Kenyatta amesema Rais wa zamani alikuwa kiongozi shupavu aliyetoa mchango wake katika kupigania uhuru wa Kenya na kutumia sehemu kubwa ya maisha yake kwa kulitumikia taifa.

XS
SM
MD
LG