Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:27

Benki Kuu ya Burundi yafunga maduka ya kubadilisha fedha za kigeni


Benki Kuu ya Burundi Ijumaa imechukuwa uamuzi wa kufuta leseni za maduka yote yanayofanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni nchini humo.

Katika barua yake Mkuu wa Benki ya Taifa, Jean Ciza aliowaandikia wamiliki wa maduka hayo amesema “ Kutokana na kukaidi agizo la benki ya taifa la kuheshimu kiwango cha ubadilishaji, na athari za mwenendo huo wa kutoheshimu sheria kwenye uchumi wa taifa, mmenyanganywa leseni za usajili mliokuwa mmpewa.”

Wamiliki wa maduka ya kubadili fedha za kigeni wametakiwa kuondoa mabango yote yenye kutangaza biashara zao yaliyoandikwa "maduka ya kubadili fedha”, mkuu wa benki ya taifa ameongeza.

Mkuu huyo amesema maduka ya kubadili fedha katika benki za biashara ndio yataendelea kufanya shughuli hizo.

Jean Ciza ameongeza kuwa hatua hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 15 ya mwezi huu wa Februari.

Burundi inakabiliwa na uhaba wa sarafu za kigeni tangu wafadhili wake kuzuia msaada wa fedha waliokuwa wanatoa kwa taifa hilo.

Umoja wa Ulaya ambao ulikuwa unachangia kwa kutoa msaada wa asilimia 50 kwenye bajeti ya serikali, ilisitisha msaada huo tangu mwaka wa 2016, ukiishtumu serikali kuvunja haki za binadamu na kukandamiza uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

Kufwatia mzozo wa kisiasa unaolikumba taifa hilo la Afrika ya kati tangu April 2015, sekta ya utalii ambayo ilikuwa inaipatishia nchi pesa za kigeni imeathirika kwa sababu watali wa kigeni hawasafiri tena kuelekea Burundi.

XS
SM
MD
LG