Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:07

Hali ya haki za bindamu bara la Afrika bado ni tete - Ripoti ya HRW


Ripoti ya shirika la kufuatilia haki za bindamu Human Rights Watch World Report 2020
Ripoti ya shirika la kufuatilia haki za bindamu Human Rights Watch World Report 2020

Kulikuwa na hasira katika bara la Afrika mwaka 2019, linasema shirika la kufuatilia haki za binadamu Human Rights Watch mwaka 2020, na inasema hakuna dalili ya hali hiyo kutulia mwaka huu.

Hasira iliyoko nchi za Afrika

Nchini Sudan na Guinea, kulijitokeza vizuizi mbalimbali na uongozi unaonang’ania madarakani. Nchini Zimbabwe, maandamano yalikuwa Zaidi juu ya hali ya uchumi. Wakati katika maeneo ya vijijini Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maandamano yalikuwa juu ya haki za jamii ambazo zimelazimika kukimbia makazi yao.

Lakini hasira ya umma ni jambo zuri kuonekana, limesema HRW katika kuzindua ripoti yake huko mjini Johannesburg.

Mkurugenzi wa uhamasishaji wa HRW, Afrika, Carine Kaneza Nantulya anasema raia wa kawaida wameangazwa mwaka 2020.

“Tumeona, nafikiri, watu wa kawaida wa bara la Afrika wakiwakilisha, wakiwa wawakilishi kwa ajili ya mabadiliko wanayotaka kuyaona , ambapo tumeoshuhudia ongezeko la maandamano ya amani katika nchi mbalimbali,” amesema. “Kitu kingine tulichokiona ni kurudi nyuma kwa serikali katika hatua iliyopiga kuimarisha uhuru wa kisiasa na kiraia.”

Mengi zaidi yanatarajiwa kutoka kwa viongozi wa Afrika

Hilo limechukuwa muelekeo wa ukandamizaji na unyanyasaji wa dhahiri unaofanywa na polisi, kama ulivyoonekana huko Afrika Kusini, amesema mtafiti wa HRW Kusini mwa Afrika, Dewa Mavhinga.

“Tulitarajia mengi zaidi kutoka kwa viongozi wa kusini mwa Afrika, akiwemo Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini, kwa misingi ya ahadi na dhamira zao kuwapa wanachi haki zao katika eneo hilo,” amesema.

“Lakini tulishuhudia kukandamizwa kwa watetezi wa haki za bindamu katika nchi kama vile Zimbabwe,” Mavhinga aliiambia Sauti ya Amerika.

“Kulikuwa na ukamataji wa waandamanaji, polisi walitumia nguvu za ziada na mihimili mingine ya vikosi vya usalama vilifanya hivyo,” amesema. Hakujakuwa na uwajibikaji wa aina yoyote.

Mavhinga alisema viongozi wa Afika wanatakiwa kufanya mabadiliko zaidi, wakati wananchi wanaleta mabadiliko wao wenyewe. Ametoa mfano wa taifa lenye katiba iliyoendelea kuliko zote katika bara la Afrika, kuwa ni Afrika Kusini, ambayo inapokea uongozi katika mzunguko wa uenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka 2020.

“Afrika Kusini inalazimika kufikia viwango,” amesema. “ Ni lazima itekeleze haki za binadamu na kutekeleza urithi aliouacha Nelson Mandela,” amesema Mavhinga. “Lakini ni juu yetu kuendelea kushinikiza hilo lifanyike,” amesema.

Matumaini Pembe ya Afrika, Sudan

Lakini kulikuwa pia na matumaini, kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia kushinda tuzo ya Nobel ya Amani kwa ajenda ya mabadiliko aliyokuja nayo na hatua za kutafuta suluhu na mahasimu wao Eriteria, amegusia mkurugenzi msaidizi wa uhamasishaji wa HRW Afrika, Babatunde Olugboji.

Aligusia tukio ambalo watu wachache wangeweza kubashiri wakati kama huu mwaka 2019 : kutokea upinzani uliopata umashuhuri uliopelekea kupinduliwa kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir baada ya kutawala kwa miaka 30 ambapo kulikuwa na ukandamizaji na uvunjifu wa haki za bindamu na jaribio la mauaji ya halaiki katika eneo la Darfur.

“Nafikiri watu wanauelewa zaidi wa haki zao,” alisema Olugboji. “Nani angeweza kufikiria Bashir angepinduliwa Sudan?

XS
SM
MD
LG