Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:03

Kenya yatakiwa kuongeza kasi dhidi ya ufisadi


Nembo ya kupambana na Rushwa ulimwenguni
Nembo ya kupambana na Rushwa ulimwenguni

Mkurugenzi Mkuu wa Transparency International nchini Kenya Samuel Kimeu amesema kuwa Kenya inafaa kuongeza kasi katika kutokomeza ufisadi na kuwachukulia hatua mafisadi na nyenendo zao.

Kenya katika miaka ya nyuma wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta imeonekana kupambana na maafisa wakuu serikalini wanaojihusisha na ufisadi, lakini bado wanafursa zaidi ya kuondoa tatizo hilo.

Kwa upande wake Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi EACC nchini Kenya imeeleza kuwa nchi hiyo imepiga hatua muhimu mno katika kutokomeza jinamizi la ufisadi.

Ripoti hiyo ya Transparency International imeiorodha Kenya kuwa ya 143 ikiwa imepanda daraja kwa pointi mbili zaidi ya kiwango cha mwaka 2016, huku Uganda ikiorodheshwa kuwa ya 151 kwa alama 26.

Ripoti hiyo vile vile imemurika mazingira ambayo waandishi wa habari wanafanya kazi na hali inayoyakabili mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Pia inaonyesha kiwango cha ufisadi katika nchi mbalimbali na kuiweka Kenya kuwa ya 143 kati ya mataifa 180 ulimwenguni.

Ripoti hiyo imeitaja Rwanda kuwa ya 48 na Tanzania 103 na kuzitaja kuwa ni nchi bora katika ukanda wa Afrika Mashariki kufuatia juhudi zao za kukabiliana na ufisadi.

Nayo Burundi imechukua nafasi ya157 na Sudan Kusini 179, zote zikiorodheshwa kuwa nchi zilizo na juhudi butu za kupambana na kutokomeza ufisadi.


XS
SM
MD
LG