Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:18

Uhuru wa kujieleza mashakani China, Misri, Uturuki- Ripoti


Amnesty international
Amnesty international

Ripoti ya kila mwaka ya shirika la haki za binadamu Amnesty International imekusanya taarifa za uvunjifu wa haki za binadamu katika nchi takriban 160 na imedai kuwa mwaka 2017 ulishuhudia siasa za chuki na vitisho ambazo ziliendelezwa na baadhi ya viongozi wenye madaraka makubwa duniani.

Katika ripoti hiyo mpya Amnesty imesema kuwa vitendo vya viongozi wa Misri, Ufilipino, Venezuela, China, Russia na Marekani zimekuwa zikikandamiza haki za mamilioni ya watu.

Viongozi hao wazi wazi wamekiuka sheria za haki za binadamu au wamewaamrisha wengine kukaidi sheria hizo. Suala la Rais wa Ufilipino [Rodrigo] Duterte yeye ameamrisha watu kutekeleza mauaji ya washukiwa wanaojihusisha na madawa ya kulevya,” mkurugenzi mtendaji wa Amnesty Margaret Huang amesema.

Ripoti hiyo pia inamkosoa Rais wa Marekani Donald Trump juu ya sera zake za uhamiaji, na ukandamizaji wa uhuru wa habari na juu ya rikodi yake juu ya haki za wanawake. VOA ilifanya juhudi za kupata maoni kutoka ikulu ya White House na Wizara ya Mambo ya Nje Marekani na hawakupata majibu yoyote.

Kama inavyojulikana rasmi kuwa ni Sera ya Jiji la Mexico, kukatazwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje Marekani na Shirika la Misaada la Marekani USAID kufadhili taasisi za kimataifa ambazo hutoa ushauri juu ya utoaji mimba ambao umekuwa ukitekelezwa na kusitishwa tangu mwaka 1984, ikitegemea ni chama gani kimechukua madaraka Ikulu ya White House.

Chini ya Rais Trump sera hiyo ilikuwa na upeo mkubwa zaidi na kugusa ufadhili wa taasisi za Kimarekani za kimataifa zinazotoa huduma za afya, kwa hoja ya kuwa katazo hilo linakusudia kuwahami watoto ambao bado hawajazaliwa.

Kwa upande wao kikundi cha kutetea haki za wanawake kimesema kuwa katazo hilo limeathiri taasisi kama yao kwa kupoteza ufadhili wa mamilioni ya dola za Kimarekani.

“Kwa hivyo tayari katika maeneo kama vile Madagascar, Uganda, Zimbabwe tumeona programu ambazo hasa zilikuwa zinawasaidia wanawake wanaokabiliwa na hali hatarishi, kama vile programu ya kutoa misaada kwa sekta binafsi ambazo zinawawezesha wanawake kuzuia kupata ujauzito zimekwama na haziwezi kufikiwa na wanawake hao,” amesema John Lotspeich, mkurugenzi wa ushirika na uhamasishaji wa rasilimali kwenye shirika la Marie Stopes International.

Lakini hata hivyo, ripoti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya mwezi huu imegundua kuwa wadau wa afya mbalimbali nje ya Marekani wamekubali matakwa ya sera hiyo mpya na kupokea ufadhili mpya.

Ripoti hiyo pia imeona tayari maeneo “ambayo yanahitaji maelekezo zaidi” na kupendekeza kupitiwa tena sera hizo ifikapo Disemba “ambapo uzoefu zaidi utawezesha kutathmini kwa kina manufaa na changamoto za sera mpya.”

Wakati huo huo Ripoti ya Amnesty imedai kuwa uhuru wa kujielezea umeathiriwa mwaka 2017 na kuonyesha wakiukaji wa uhuru huo wakuu kuwa ni China, Misri na Uturuki. VOA ilijaribu kuwatafuta wasemaji wa balozi za nchi hizo zilizoko Marekani lakini bado hawajatoa majibu yoyote.



XS
SM
MD
LG