Athari za Kimbunga Idai : Miili zaidi yaendelea kuopolewa Msumbiji

Familia zilizopoteza makazi yao kutokana kimbunga Idai wakiokolewa katika wilaya ya Buzi iliyokumbwa na mafuriko maili 120 nje ya mji wa Beira, Rufiji, Machi 23, 2019.

Mashirika ya kutoa misaada yanayoshughulikia kutafuta watu waliotoweka kutokana na kimbunga Idai, katikati ya nchi ya Msumbiji, yanaendelea kuopoa miili zaidi ya watu waliokufa kutokana na janga hilo.

Kimbunga hicho kilisababisha uharibifu mkubwa katika nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe na jumla ya watu 783 walipoteza maisha yao.

Wakati huohuo Msumbiji imeripoti matukio 138 vya maambukizi ya kipindupindu katika mji wa Beira, huku jumla ya watu 800,000 wakiwa wamewekewa utaratibu wa kupatiwa chanjo dhidi ya kipindupindu.

Watu 150,000 wameachwa bila makao kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga hicho huku 140,000 wakiwa wanaishi katika kambi za muda.

Maafisa wanasema wanatarajia kwamba watu milioni moja laki nane waliathiriwa na kimbunga hicho.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.