Thailand yautaka utawala wa kijeshi Myanmar kupunguza ghasia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Parnpree Bahiddha –Nukara

Thailand imetuma ujumbe kwa utawala wa kijeshi Myanmar ili  kupunguza ghasia, waziri wake wa mambo ya nje amesema leo.

Waziri huyo ameongeza kuwa maandalizi yanaendelea kwa watu wanaomiminika kuvuka kuingia nchini Thailand baada ya mji wa mpakani kuchukuliwa na waasi.

Parnpree Bahiddha –Nukara amesema Thailand ilikuwa pia inafanya kazi na wajumbe wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN, kufuatia mpango wa amani uliokwama kwa ajili ya Myanmar , unaojulikana kama “ makubaliano yake ya pointi tano”.

Mgogoro wa maji nchini Myanmar.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Parnpree Bahiddha –Nukara anaeleza:

“Kinachotutia wasi wasi ni tunataka kuona amani huko Myawaddy, sio tu kwa sababu ya biashara tulizonazo na wao lakini ni kwa sababu ni nchi yetu jirani na hatutaki kuona ghasia na tunataka kuwaona wakizungumza pamoja, wanaweza kututumia sisi kama wapatanishi kama wanataka.”

Wakazi wa Myanmar wakivuka daraja la 1st Thai-Myanmar Friendship Bridge wilaya ya Myawaddy masharika ya Myanmar, April 12, 2024.