Jeshi la Arakan lilihamia Pauktaw, mji wa watu 20,000 karibu na bandari muhimu ya kina kirefu katika mji mkuu wa jimbo la Rakhine magharibi, mnamo Novemba 15.
Ilifungua mkondo mpya katika mashambulio kwa makabila madogo kaskazini mwa Myanmar ambayo yameghadhibisha jeshi la serikali, kukata njia za biashara kuelekea China jirani na kusababisha zaidi ya watu 330,000 kuhama makazi tangu mwezi uliopita.
Pauktaw imekuwa moja ya maeneo yanayo zozaniwa na wakaazi waliowasiliana na AFP siku ya Jumatano waliripoti mapigano makali ndani na nje ya mji huo, ambao ni kilomita 25 kutoka Sittwe, mji mkuu wa jimbo hilo.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.
Forum