Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:18

Wakimbizi wa Rohingya wana shaka na juhudi za China kuwarejesha Myanmar


Watoto wawili wa Rohingya wakiwa katika kambi ya wakimbizi isiyokuwa na miundombinu na chafu katika mji wa Cox's Bazar, Bangladesh, Juni 9, 2023. (Noor Hossain/VOA)
Watoto wawili wa Rohingya wakiwa katika kambi ya wakimbizi isiyokuwa na miundombinu na chafu katika mji wa Cox's Bazar, Bangladesh, Juni 9, 2023. (Noor Hossain/VOA)

Wakimbizi wa Rohingya wanaoishi katika kambi chafu huko Bangladesh wana  mashaka  kwa juhudi za China kusaidia kuwarejesha Myanmar, ambako walikuwa wanakabiliwa na njama za mauaji na kuchomwa moto na majeshi hayo hayo ambayo yanatawala nchini humo.

“Tunataka kurejea nyumbani. Lakini, chini ya mpango huu wa majaribio, jeshi la Myanmar litatulazimisha kuishi katika kambi. Hawata turuhusu kurejea majumbani na vijijini kwetu,” Aung Myaing, mfanyakazi wa kujitolea wa Rohingya katika kambi ya wakimbizi ya Kutupalong huko Cox Bazar, Bangladesh, aliiambia VOA kwa njia ya simu.

“Tunahisi hatua ya China kuingilia kati suala hili la kurejeshwa Warohingya linaushawishi wa maslahi binafsi ya China kuliko wasi wasi kwa wakimbizi walioko hapa. Iwapo China inataka kweli kusaidia, inalazimika kuhakikisha kuwa Warohingya wanarejea katika hali ya usalama na kupewa heshima wanayostahili,” alisema.

Takriban Warohingya milioni 1 wanaishi katika kambi kwenye mpaka wa wilaya ya Cox Bazar, wengi wao wakiwa wamekimbia msako uliokuwa ukifanywa na jeshi huko Myanmar mwaka 2017, na hivi sasa ikiwa ni suala lililofunguliwa kesi ya mauaji ya kimbari katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC.

Zaidi ya miaka miwili tangu mapinduzi ya kijeshi kutokea Myanmar, China imerejesha uhusiano wa karibu na wanajeshi wanaotawala hivi sasa.

Mnamo Julai 27, wakati wa ziara ya kushtukiza ya siku mbili Myanmar, mwakilishi maalum wa China Deng Xijun alikutana na maafisa muhimu wa jeshi, akiwemo Jenerali Mwandamizi Min Aung Hlaing.

Jenerali Mwandamizi Min Aung Hlaing Jan. 31, 2023, ofisi ya habari ya jeshi la Myanmar.
Jenerali Mwandamizi Min Aung Hlaing Jan. 31, 2023, ofisi ya habari ya jeshi la Myanmar.

“Tulikuwa na mazungumzo ya kina kuhusu mchakato wetu wa amani, utulivu wa eneo la mpakani kati ya China na Myanmar, na masuala ya usalama na ulinzi,” msemaji wa utawala wa kijeshi Meja Jenerali Zaw Min Tun aliiambia VOA kwa njia ya simu.

Wawakilishi wa China, akiwemo Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Qin Gang, walifanya ziara mara kadhaa huko Myanmar mwaka huu.

Kulingana na wachambuzi, ziara za mara kwa mara ni ishara kuwa China inafanya juhudi ya kutekeleza tena miradi yake mikubwa ya uwekezaji huko.

Mnamo mwezi Januari, China ilianzisha tena mazungumzo na Bangladesh juu ya mradi wa majaribio wa kuwarejesha nyumbani Warohingya wasiokuwa na makazi.

Mwezi Aprili, Deng aliitembelea Dhaka na kujadili na Waziri wa Mambo ya Nje AK Abdul Momen na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje juu ya kurejeshwa kwa Wakimbizi wa Rohingya.

Mwezi huo huo, China ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa pande tatu (China, Myanmar na Bangladesh) wa kuwarejesha warohingya, mkutano ulifanyika huko Kunming, mji mkuu wa jimbo la Yunnan.

Forum

XS
SM
MD
LG