Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:19

Rais wa Indonesia Joko Widodo ni mwenyeji wa mkutano wa ASEAN unaoanza wiki hii


Rais wa Indonesia Joko Widodo ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa ASEAN nchini mwake
Rais wa Indonesia Joko Widodo ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa ASEAN nchini mwake

Masuala ya mgawanyiko yanatawala bila ya dalili ya kupatikana suluhisho ikiwemo mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe unaoleta maafa huko Myanmar, mzozo mpya umeibuka  katika South China Sea, na upinzani wa muda mrefu wa Marekani na China. Mikutano ya mataifa ya ASEAN itafunguliwa Jumanne mjini Jakarta.

Viongozi wa Asia Kusini Mashariki wakiongozwa na mwenyeji wao Rais wa Indonesia Joko Widodo wanakusanyika kwa mkutano wao wa mwisho mwaka huu, huku masuala ya mgawanyiko yakiwepo bila ya dalili ya kupatikana suluhisho.

Mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe unaoleta maafa huko Myanmar, mzozo mpya umeibuka katika South China Sea, na upinzani wa muda mrefu wa Marekani na China. Mikutano ya Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) itafunguliwa Jumanne katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta chini ya ulinzi mkali.

Kutokuwepo kwa Rais wa Marekani Joe Biden ambaye kwa kawaida anahudhuria mkutano huo kunaongeza hali ya isiyo ya kawaida ambapo tayari kuna nchi 10 katika umoja huo na mshikamano. Mawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN walikusanyika Jumatatu kukamilisha ajenda ya viongozi hao.

Waziri wa mambo ya nje wa Indonesia Retno Marsudi amekiri hali ngumu katika eneo hilo ambalo jumuiya hiyo ilikuwa inakabiliwa nayo na inapaswa kushinda, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Myanmar. Mpango wa Pointi tano uliobuniwa na viongozi mwaka 2021 kusaidia kuirudisha Myanmar katika hali ya kawaida utafanyiwa tathmini, alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG