Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 20:53

Boti iliyowabeba wakimbizi wa Rohingya imeonekana magharibi mwa Indonesia

Boti iliyobeba wakimbizi wa Rohingya. Jimbo la Aceh. 16 November 2023. (Foto: AMANDA JUFRIAN/AFP)
Boti iliyobeba wakimbizi wa Rohingya. Jimbo la Aceh. 16 November 2023. (Foto: AMANDA JUFRIAN/AFP)

Kundi la watu takribani 250 kutoka jamii ya walio wachache walioteswa huko Myanmar waliwasili katika jimbo la Aceh siku ya Alhamisi, lakini wakaazi waliwaambia wasiingie katika eneo hilo.

Boti iliyokuwa imewabeba wakimbizi wa Rohingya ambayo ililazimika kurudi baharini mapema wiki hii ilionekana Jumamosi maili kadhaa kutoka pwani ya mkoa wa magharibi wa Indonesia, kulingana na kamanda wa eneo hilo.

Kundi la watu takribani 250 kutoka jamii ya walio wachache walioteswa huko Myanmar waliwasili katika jimbo la Aceh siku ya Alhamisi, lakini wakaazi waliwaambia wasiingie katika eneo hilo.

Boti hiyo ilisafiri hadi eneo jingine katika jimbo la Aceh ambako kundi la pili la wakaazi liliwarudisha baharini siku ya Alhamisi. Kamanda wa jeshi la majini katika mji wa Lhoksemauwe mjini Aceh, ameliambia shirika la habari la AFP leo Jumamosi kwamba boti hiyo ilionekana “leo asubuhi” na “inaonekana kufanana” na ile iliyorudishwa Alhamisi, akiongeza kwamba ilikuwa ikielekea mashariki.

Forum

XS
SM
MD
LG