Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:15

Wahamiaji zaidi ya 100 wametoroka katika kituo cha wahamiaji huko Malaysia


Mfano wa wahamiaji wa Rohingya
Mfano wa wahamiaji wa Rohingya

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Ruslin Jusoh alisema wafungwa 131 walitoroka kwenye kituo katika jimbo la Perak

Zaidi ya wahamiaji 100 wa Rohingya wametoroka kutoka kituo cha kuwazuilia wahamiaji nchini Malaysia baada ya maandamano, huku mmoja akithibitishwa kufariki katika ajali ya barabarani, maafisa wamesema Ijumaa. Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili ambapo tukio kama hilo lilitokea.

Mwaka 2022, wakimbizi 528 wa Rohingya walifanya maandamano na kutoroka kutoka kizuizini katika jimbo la kaskazini la Penang. Sita waliuawa wakati wakijaribu kuvuka barabara kuu, na wengine kadhaa walikamatwa tena.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Ruslin Jusoh alisema katika taarifa kwamba wafungwa 131 walitoroka kutoka kituo kimoja katika jimbo la Perak Alhamisi jioni. Alisema mmoja wa wafungwa hao aliuawa katika ajali ya barabarani.

Takriban wafanyakazi 400 walipelekwa ili kuwatafuta, aliongeza bila kutoa maelezo juu ya kile kilichosababisha kuzuka kwa tukio hilo. Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo Mohamad Naim Asnawi alinukuliwa na shirika la habari la Bernama akisema wahamiaji hao walitoroka kutoka kwenye kizuizi cha wanaume hao baada ya ghasia kuzuka katika kituo hicho.

Washukiwa hao ni pamoja na Wa-Rohingya 115 na raia 16 wa Myanmar, wote wakiwa wanaume.

Forum

XS
SM
MD
LG