Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:57

Mashambulizi ya anga ya jeshi la Myanmar yameuwa raia 17


Ramani ya Myanmar na maeneo jirani zake
Ramani ya Myanmar na maeneo jirani zake

Mashambulizi ya anga katika kijiji cha Kanan kusini mwa mpaka wa India pia yaliwajeruhi watu 20 kulingana na kundi la haki za binadamu.

Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Myanmar katika kijiji kinachodhibitiwa na waungaji mkono wa demokrasia huko kaskazini magharibi mwa nchi yamesababisha vifo vya raia angalau 17, wakiwemo watoto tisa, wakaazi wa eneo hilo na kundi la haki za binadamu limesema Jumapili.

Mashambulizi ya anga ya asubuhi katika kijiji cha Kanan kwenye mji wa Khampat katika mkoa wa Sagaing, kusini mwa mpaka wa India, pia yaliwajeruhi watu 20 walisema.

Myanmar inakabiliwa na ghasia zilizoanza baada ya jeshi kuiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa ya Aung San Suu Kyi hapo Februari 2021. Baada ya maandamano ya amani kusitishwa kwa nguvu za kijeshi, wapinzani wengi wa utawala wa kijeshi walibeba silaha, na sehemu kubwa ya nchi hivi sasa imegubikwa na mgogoro.

Vyombo huru vya habari vya mtandaoni nchini humo na idhaa ya BBC ya Myanmar vimeripoti shambulio hilo la anga siku ya Jumapili, lakini serikali ya kijeshi ilikanusha kuhusika, ikidai kuwa ni habari za uongo zilizoenezwa na Khit Thit Media, shirika huru la habari la mtandaoni linalounga mkono upinzani dhidi ya jeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG