Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:04

Malaysia: Zaidi ya Warohingya 100 watoroka kizuizini, msako mkali wafanyika


Wakimbizi wapya Warohingya wakipumzika mara baada ya kuwasili katika pwani ya Kuala Parek huko East Aceh February 1, 2024.
Wakimbizi wapya Warohingya wakipumzika mara baada ya kuwasili katika pwani ya Kuala Parek huko East Aceh February 1, 2024.

Zaidi ya wahamiaji Warohingya 100 wametoroka kutoka katika kituo cha kizuizi nchini Malaysia baada ya maandamano, mtu mmoja akithibitishwa kupoteza maisha katika ajali ya barabarani, maafisa walisema Ijumaa.

Hii ilikuwa ni mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili kwamba utoro huu umetokea. Mwaka 2022, wakimbizi Warohingya 528 walifanya maandamano na kutoroka kutoka kizuizini huko kaskazini mwa jimbo la Penang.

Sita walifariki wakati wakijaribu kuvuka barabara kuu, na wengi wengineo walikamatwa tena.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Ruslin Jusoh alisema katika taarifa yake kuwa wafungwa 131 walitoroka kutoka katika kituo kimoja huko jimbo la Perak Alhamisi usiku. Alisema mmoja kati ya waliokuwa kizuizini alifariki katika ajali ya barabarani.

Mkuu wa polisi wa wilaya Mohamad Naim Asnawi amekaririwa na shirika la habari la taifa Bernama akisema kuwa wahamiaji hao walitoroka kutoka jengo la wanaume baada ya ghasia kuibuka katika kituo hicho.

Washukiwa hao ni pamoja na Warohingya 115 na raia wa Myanmar 16, wote wanaume, alisema.

Malaysia, ambayo ina idadi kubwa ya Waislam, ni nchi inayopendelewa na Waislam Warohingya wanaokimbia Mabuda waliowengi huko Myanmar au wale wanaokwepa hali ngumu katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh.

Malaysia haitoi hadhi ya ukimbizi, lakini inawaweka takriban wakimbizi 180,000 na wanaotafuta hifadhi wanaotambuliwa na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, wakiwemo zaidi ya Warohingya 100,000 na makundi mengine ya kikabila ya Myanmar. Maelfu wanakaa nchini humo kinyume cha sheria baada ya kuwasili kwa njia ya bahari.

Forum

XS
SM
MD
LG