Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:20

Mamilioni ya wakimbizi wa Rohingya wanaendelea kuteseka pasipo kujua pa kwenda


Wakimbizi wa Rohingya wakipokea matibabu baada ya kuwasili katika kijiji cha Maunasah Ujong Pie, Aceh, Indonesia Dec 26, 2022
Wakimbizi wa Rohingya wakipokea matibabu baada ya kuwasili katika kijiji cha Maunasah Ujong Pie, Aceh, Indonesia Dec 26, 2022

Boti yenye wakimbizi 185 wa Rohingya imewasili katika jimbo la Aceh, nchini Indonesia, leo Jumapili.

Mamia ya wakimbizi waliwasili mwaka uliopita kutokana na hali mbaya katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh.

Zaidi ya nusu ya wakimbizi hao waliowasili saa nane na nusu mchana, kwa saa za Indonesia, ni wanawake na Watoto.

Wengi wao wameonekana wakiwa wamelala kwenye mchanga kutokana na uchovu.

Mamia ya wakimbizi wa Rohingya wamekuwa wakiwasili Aceh katika miezi ya hivi karibuni.

Wakimbizi 174 waliwasili sehemu hiyo mnamo mwezi Desemba mwaka uliopita.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, lilisema kwamba mwaka 2022 huenda ulikuwa hatari sana kwa wakimbizi wa Rohingra ambao wamepitia mateso mabaya sana nchini Myanmar, yenye idadi kubwa ya wabudha.

Kwa miaka mingi, wakimbizi wa Rohingya wamekuwa wakitorokea katika nchi jirani za Thailand na Bangladesh na katika nchi zenye idadi kubwa ya waislamu kama Malaysia na Indonesia.

Karibu warohingya milioni 1 wanaishi katika kambi zenye hali duni ya maisha nchini Bangladesh, walikotorokea kufuatia msako mkubwa wa jeshi la Myanmar.

XS
SM
MD
LG