Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:14

Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Myanmar


Wapiganaji wa vikosi vya Mandalay People’s Defense Forces (MDY-PDF) wanaokabiliana na utawala wa kijeshi wa Myanmar.
Wapiganaji wa vikosi vya Mandalay People’s Defense Forces (MDY-PDF) wanaokabiliana na utawala wa kijeshi wa Myanmar.

Marekani itaongeza vikwazo zaidi kwa uongozi wa kijeshi wa Myanmar, miaka mitatu baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, 2021, wakati ikijumuisha watu wanne pamoja na makampuni mawili yanayohusishwa na mapinduzi hayo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kwamba hatua hiyo ya karibuni zaidi inalenga vyanzo vya fedha vinavyounga mkono utawala huo wa kijeshi dhidi ya raia wake, pamoja na wale wanaofadhili utengenezaji wa silaha ndani ya Myanmar, inayojulikana pia kama Burma.

Jumatano wizara ya Fedha ya Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya makampuni ya Shwe Byain Phyu, mmiliki wake Thein Win Zaw, pamoja na mke wake na watoto wao wawili. Vikwazo pia vimetangazwa dhidi ya kampuni ya Myanma Five Star, inayojishugulisha na safari za meli.

Wizara hiyo iliongeza kusema kwamba makampuni hayo mawili yamesaidia utalawa wa kijeshi kupata fedha za kigeni, pamoja na uagizaji wa mafuta na bidhaa nyingine kupitia ushirikiano wao wa karibu na kampuni ya umma inayomilikiwa na serikali ya Myanma Economic Holdings, au MEHL.

Taarifa zimeongeza kusema kwamba Marekani imeweka vikwazo kwa mali zinazomilikwa na walengwa, wakati wamarekani kwa ujmla wakikatazwa kufanya biashara nao.

Forum

XS
SM
MD
LG