Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 01:27

Zelenskyy atoa wito Ulaya isitishe biashara zote na Russia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (Ukrainian Presidential Press Office via AP)
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (Ukrainian Presidential Press Office via AP)

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ametoa wito kwa viongozi wa Ulaya kusitisha biashara zote na Russia, katika juhudi za kuishinikiza Moscow kuacha kuishambulia nchi hiyo kivita.

Katika ujumbe wa video, Zelenskyy amewataka viongozi wa Ulaya kufunga bandari zake kwa bidhaa kutoka Russia, kutoiuzia Russia bidhaa, kuzuia usafirishaji wa nshati miongoni mwa mengine, akiwaomba kutofanya kile amekitaja kama kufadhili vita dhidi ya Ukraine.

Katika ujumbe wa moja kwa moja kwa Ujerumani, Zelensky amesema kwamba nchi hiyo ina nguvu sana na uwezo wa mkubwa wa kuhakikisha kwamba vita dhidi ya Ukraine vinakoma.

Ombi lake linakuja wakati nchi kadhaa za Ulaya yakiwemo mataifa ya Baltic, yakitaka ununuzi wa mafuta na gesi kutoka Russia kupigwa marufuku.

Ujerumani imepinga hatua ya kupiga marufuku ununuzi wa nishati kutoka Russia.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana Jumatatu kujadili vita vya Ukraine na namna ya kuongeza vikwazo dhidi ya Russia.

Msemaji wa serikali ya Russia Dmitry Peskov ameyaonya mataifa ya Ulaya kwamba hatua ya kuweka marufuku uuzaji wa mafuta yake itaathiri kila mtu na kuleta athari mbaya sana kwa kila mtu duniani.

Marekani imetangaza marufuku ya ununuzi wa mafuta na gesi ya Russia, huku Uingereza ikisema kwamba itasitisha ununuzi wa mafuta ya Russia kufikia mwishoni mwa mwaka 2022.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

XS
SM
MD
LG