Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:53

Biden amtahadharisha Xi kutoisaidia Russia katika mazungumzo kupitia mtandao


Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mazungumzo kwa njia ya mtandao na mwenzake Rais wa China Xi Jinping. (AP Photo/Susan Walsh, File)
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mazungumzo kwa njia ya mtandao na mwenzake Rais wa China Xi Jinping. (AP Photo/Susan Walsh, File)

Mazungumzo kwa njia ya video – ya kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu uvamizi – yalidumu kwa takriban saa mbili, kulingana na White House. Wakati wa mazungumzo Biden alieleza kwa upana uwezekano “matokeo na adhabu” iwapo Beijing itachukua hatua kuwapatia Russia msaada wa vifaa.

Maafisa wa utawala wa Biden walikataa kueleza hadharani ni adhabu gani ambazo zinaweza kuchukuliwa.

“Rais Biden alimueleza Rais Xi kwa kirefu jinsi mambo yalivyoendelea kufikia hivi sasa, tathmini yake ya hali ilivyo na Rais Biden alisisitiza kupatikana kwa suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huu,” afisa wa ngazi ya juu wa utawala amewaambia waandishi wa habari kilichozungumziwa katika mazungumzo hayo.

Afisa huyo alikataa kujibu swali la VOA iwapo Biden alikuwa hana au anayo matumaini zaidi juu ya msimamo wa Beijing kwa Ukraine baada ya mazungumzo yake na Xi.

Mazungumzo hayo yalikuwa kuhakikisha kuwa kuna mazungumzo ya moja kwa moja, ya wazi na yenye maelezo ya kutosha katika ngazi ya uongozi,” afisa huyo alisema.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alithibitisha ripoti za vyombo vya habari mapema wiki hii kwamba huenda China ikachukua hatua ya kuisaidia Russia.

“Tuna wasiwasi kuwa wanafikiria moja kwa moja kuisaidia Russia vifaa vya kijeshi ambavyo vitatumiwa Ukraine,” Blinken alisema katika maelezo yake. Hakutoa ushahidi wa madai hayo, ambayo Moscow na Beijing wameyakanusha.

Wakati huo huo, kulingana na muhtasari wa mazungumzo ya simu uliotolewa Beijing, Xi alimhakikishia Biden kuwa nchi yake haitaki vita vya Ukraine viendelee.

“Rais Xi alieleza kuwa China haitaki kuona hali hii ya Ukraine ifikie hapa,” taarifa hiyo ilieleza. “Pande zote zinatakiwa kwa pamoja kuzisaidia Russia na Ukraine kuwa na mazungumzo.”

Beijing awali ilisema kuwa shutuma kuwa inaisaidia Moscow zilipangwa kuhamisha lawama

“Kauli ya kuwa China ilijua hilo, ilikubali au kuunga mkono kimya kimya vita hivi ni taarifa za zisizo sahihi,” Qin Gang, balozi wa China nchini Marekani, alieleza katika makala ya maoni iliyochapishwa katika gazeti la The Washington Post wiki hii.

Msimamo rasmi wa China juu ya uvamizi wa Moscow umekuwa kuzifikia pande zote, bila ya kuunga mkono kikamilifu wala kupinga moja kwa moja. Beijing inasema inatambua uhuru wa Ukraine, lakini inakiri kuwa upanuzi wa himaya ya NATO umeibua wa wasiwasi “halali” wa usalama kwa Russia.

XS
SM
MD
LG