Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:41

Russia yasema ina dhamira ya kufikia makubaliano ya amani na Ukraine.


Wajumbe wa Russia na Ukraine wakifanya mazungumzo karibu na mpaka kati ya Poland na Belarus, Machi 7, 2022. Picha ya AP.
Wajumbe wa Russia na Ukraine wakifanya mazungumzo karibu na mpaka kati ya Poland na Belarus, Machi 7, 2022. Picha ya AP.

Kremlin imesema Alhamisi kwamba inaweka nguvu zake zote kwenye mazungumzo ili kupatikane makubaliano ya amani na Ukraine, jambo ambalo litaipelekea Russia kusitisha operesheni za kijeshi nchini humo.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema “ Ujumbe wetu unafanya juhudi kubwa na unaonyesha utashi wa kufikia makubaliano kuliko upande mwengine”.

“Kufikia mkataba, kuheshimu vipengele vyake vyote na kuutekeleza itasimamisha mara moja kinachofanyika huko”, ameongeza.

Alipoulizwa kuhusu ripoti ya gazeti la Financial Times kwamba Russia na Ukraine zimepiga hatua kubwa katika mpango wa amani wa muda, Peskov amesema “ Si sahihi, kuna mambo ambayo ni kweli, lakini kwa ujumla sio sahihi”.

XS
SM
MD
LG