Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:04

Ukraine yaitaka Moscow kuchukulia mazungumzo ya amani kwa dhati


Ukraine's President Zelenskiy is seen during a call with U.S. President Biden in Kyiv
Ukraine's President Zelenskiy is seen during a call with U.S. President Biden in Kyiv

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine kwa mara nyingine tena Jumamosi, ametoa wito kwa Moscow, “kuchukulia kwa dhati mazungumzo ya amani”, akisema “hiyo ndio nafasi pekee kwa Rashia kupunguza hasara kubwa iliofanya kutokana na makosa yake mwenyewe.”


Pande zote mbili kwa hivi sasa zinaendelea na mazungumzo kupitia mtandao, lakini hadi sasa, kama duru zilizopita, hakuna mafanikio yaliopatikana.


Mpatanishi mkuu wa Ukraine kwenye mazungumzo hayo Mykhailo Podolyak, kwenye ujumbe wa Twitter Jumamosi, amesema ni lazima kwa China kuchukua uwamuzi ulosahihi na kuungana na mataifa ya dunia kulaani uvamizi wa kikatili wa Rashia nchini Ukraine.


Podolyak alitoa wito huo siku moja baada ya Rais Joe Biden kumhimiza Rais Xi Jingping wa China kupitia mazungumzo ya simu, kujiunga na Jumuia ya Kimataifa kulaani uvamizi wa Rashia na kutoisiadia Moscow la sivyo itakabiliwa na hasara kubwa.


Kwa upande wake Rashia imedai Jumamosi, kwamba imefyetua makombora yanayo kwenda kwa kasi dhidi ya ghala ya silaha chini ya ardhi nchini Ukraine. Ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kutumia makombora hayo mapya ya hypersonic, katika vita.


Msemaji wa jeshi la anga la Ukraine Yuri Ignat, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ghala lake la silaha katika kijiji cha Deliatyn, karibu na mpaka wa Romania limeshambuliwa na kusababisha hasara kubwa.


Karibu miili ya wanajeshi 50 wa Ukraine zimepatikana katika kambi karibu na ghala hiyo ambapo inasemekana kulikuwepo na wanajeshi 200 walokua wamelala.

XS
SM
MD
LG