Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:53

Majeshi ya Russia yaliyokata tamaa yapiga mabomu, na kutumia makombora mapya

FILE - MiG-31K fighter ya jeshi la anga la Russia inayobeba kombora aina ya Kinzhal Russia. (Picha na Wizara ya Ulinzi ya Russia na AFP).

Maafisa wa jeshi la Russia wamesema Jumamosi kwamba walirusha makombora ya hypersonic kwa mara ya kwanza kuelekea Ukraine kulenga kile walichosema ni maeneo ya kuhifadhi silaha chini ya ardhi katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo.

Makombora ya Kinzhal yanasafiri kwa kasi sana, ya Mach 9, yana uwezo wa kukwepa kuonekana na mifumo ya ulinzi, na walipokuwa wanatangaza utengenezaji wa makombora hayo mwaka 2019, Rais wa Russia Vladimir Putin alielezea kuwa “hayaonekani.”

Mfumo wa makombora hayo ya Kinzhal wenye makombora ya masafa ya mbali ya anga yenye kasi zaidi yaliharibu idadi kubwa ya makombora na silaha za anga zilizokuwa katika ghala chini ya ardhi katika kijiji cha Deliatyn huko mkoa wa Ivano-Frankivsk,” Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema Jumamosi.

Shambulizi hilo lilifanyika Ijumaa, lakini madai ya Russia hayakuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.

Maafisa wa jeshi Ukraine wanasema kuwa matumizi ya makombora ya Kinzhal yanazidi kuonyesha kuwa Russia imeshindwa kufikia malengo yake ya kimkakati wa kivita kwa kutumia majeshi ya ardhini na hivyo inaendeleza kwa nguvu zote vyote viwili mashambulizi ya mabomu katika miundombinu ya raia na matumizi ya silaha zenye uwezo wa kupiga sehemu maalum ili kujaribu kuitisha Ukraine na kuwakatisha tamaa kutopambana na Russia.

Watumishi wa Jeshi la Ukraine wamesema Jumamosi Russia ilikuwa imepiga makombora 14 na kufanya mashambulizi ya anga 40 katika maeneo mbalimbali, hususan maeneo ya raia, kote Ukraine katika kipindi cha saa 24.

Wamethibitisha madai ya Russia kuwa wanajeshi wake wameingia katikati ya mji wa bandari wa Mariupol uliozingirwa kusini mwa Ukraine, ambao umeshambuliwa kwa mabomu na kunyimwa chakula kwa siku kadhaa katika udhibiti wa mji huo uliowaacha wakazi 300,000 wakiwa na chakula na maji kidogo na bila ya umeme na intaneti.

Miili ya watu imeachwa barabarani au ikiwa imefunikwa kwenye roshani za nyumba. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumamosi kwamba mji huo ulikuwa unakabiliwa “hali mbaya sana katika historia yake, katika historia ya Ukraine.”

Meya wa Mariupol, Vadym Boichenko, alijitokeza kuthibitisha madai ya Russia ya majeshi yake kuingia ndani ya mji huo, akisema upinzani wa mapambano ulikuwa unaendelea ambako yeye amejificha.

Uharibifu uliofanywa na mashambulizi ya Russia mjini Mariupol nchini Ukraine kama yalivyopigwa picha kutoka angani na kamera za Satellite. (Satellite image ©2022 Maxar Technologies via AP).

Wakati Mariupol ikiwa inaelekea kutekwa na Russia, Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi amekiri kuwa wamepoteza mawasiliano na eneo la Sea of Azov “kwa muda” kwa sababu majeshi ya Russia wamefanikiwa kuimarisha wao kuzunguka Mariupol..

Lakini wakati majeshi ya Russia yakiendelea kupiga hatua katika upande wa kusini wa nchi hiyo, iwapo wamesitishwa, bado wamekwama katika enoe la kaskazini la nchi hiyo na inawezekana wamekata tamaa kujaribu kuingia kwa nguvu Kyiv.

Makombora ya Kinzhal yanasafiri kwa kasi sana, ya Mach 9, yana uwezo wa kukwepa kuonekana na mifumo ya ulinzi, na walipokuwa wanatangaza utengenezaji wa makombora hayo mwaka 2019, Rais wa Russia Vladimir Putin alielezea kuwa “hayaonekani.”

Mfumo wa makombora hayo ya Kinzhal wenye makombora ya masafa ya mbali ya anga yenye kasi zaidi yaliharibu idadi kubwa ya makombora na silaha za anga zilizokuwa katika ghala chini ya ardhi katika kijiji cha Deliatyn huko mkoa wa Ivano-Frankivsk,” Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema Jumamosi.

Shambulizi hilo lilifanyika Ijumaa, lakini madai ya Russia hayakuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.

Maafisa wa jeshi Ukraine wanasema kuwa matumizi ya makombora ya Kinzhal yanazidi kuonyesha kuwa Russia imeshindwa kufikia malengo yake ya kimkakati wa kivita kwa kutumia majeshi ya ardhini na hivyo inaendeleza kwa nguvu zote vyote viwili mashambulizi ya mabomu katika miundombinu ya raia na matumizi ya silaha zenye uwezo wa kupiga sehemu maalum ili kujaribu kuitisha Ukraine na kuwakatisha tamaa kutopambana na Russia.

Watumishi wa Jeshi la Ukraine wamesema Jumamosi Russia ilikuwa imepiga makombora 14 na kufanya mashambulizi ya anga 40 katika maeneo mbalimbali, hususan maeneo ya raia, kote Ukraine katika kipindi cha saa 24.

Wamethibitisha madai ya Russia kuwa wanajeshi wake wameingia katikati ya mji wa bandari wa Mariupol uliozingirwa kusini mwa Ukraine, ambao umeshambuliwa kwa mabomu na kunyimwa chakula kwa siku kadhaa katika udhibiti wa mji huo uliowaacha wakazi 300,000 wakiwa na chakula na maji kidogo na bila ya umeme na intaneti.

Miili ya watu imeachwa barabarani au ikiwa imefunikwa kwenye roshani za nyumba. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumamosi kwamba mji huo ulikuwa unakabiliwa “hali mbaya sana katika historia yake, katika historia ya Ukraine.”

Meya wa Mariupol, Vadym Boichenko, alijitokeza kuthibitisha madai ya Russia ya majeshi yake kuingia ndani ya mji huo, akisema upinzani wa mapambano ulikuwa unaendelea ambako yeye amejificha.

Wakati Mariupol ikiwa inaelekea kutekwa na Russia, Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi amekiri kuwa wamepoteza mawasiliano na eneo la Sea of Azov “kwa muda” kwa sababu majeshi ya Russia wamefanikiwa kuimarisha wao kuzunguka Mariupol.

XS
SM
MD
LG