Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:19

Rais wa Ukraine aomba msaada zaidi kutoka Marekani


Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi, D-Calif., akimkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kulihutubia Bunge la Marekani katika jengo la Congress, Washington, Jumatano, Machi 16, 2022. (AP Photo/J. Scott Applewhite, Pool)
Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi, D-Calif., akimkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kulihutubia Bunge la Marekani katika jengo la Congress, Washington, Jumatano, Machi 16, 2022. (AP Photo/J. Scott Applewhite, Pool)

Rais wa Ukraine Jumatano amewasihi wabunge wa Marekani kuchukua hatua zaidi kulilinda taifa lake katikati ya mashambulizi yanayofanywa na majeshi ya Russia kwa wiki tatu sasa, ikikumbushia baadhi ya huzuni mbaya katika historia ya Marekani.

Rais Volodymyr Zelenskyy ameliomba Bunge la Marekani na Rais Biden kutoa misaada zaidi ya kijeshi na kuweka marufuku ya kutoruka ndege katika anga zilizozingirwa za Ukraine.

Russia imeendelea kuushambulia mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Jumatano, wakati mawaziri wa NATO wakikusanyika huko Ulaya kujadili uvamizi wa Russia.

“Hivi sasa, hatma ya nchi yetu inaamuliwa,” Rais wa Ukraine alisema, akiongea kwa njia ya mtandao kwenye kikao kilichokuwa kimejaa wabunge wa Marekani wakisikiliza hotuba iliyoibua kumbukumbu zenye kusikitisha za shambulizi la Japan mwaka 1941 huko Pearl Harbor, iliyo isukuma Marekani kuingia Vita vya Pili vya Dunia; na shambulizi la kigaidi la Septemba 11, 2001, iliyoifanya Marekani kuanzisha vita duniani dhidi ya ugaidi katika maeneo mbalimbali vilivyoendelea kwa miongo miwili.

Historia ya Marekani

Muigizaji aliyegeuka kuwa Rais mwenye umri wa miaka 44, aliyezungumza Kiingereza kwa sehemu ya hotuba yake, pia katika hotuba iliibua historia ya Marekani zilizohamasisha, ikiwemo maneno ya kiongozi wa haki za raia Martin Luther King, Jr.

“Ninalazimika kulinda anga zetu,” alisema Zelenskyy. “Ninataka maamuzi yenu, msaada wenu, ikimaanisha uhalisi wa kitu kilekile, kile mnachohisi nyie mnaposikia maneno ‘mimi nina ndoto.’”

Alisisitiza ombi lake la marufuku ya kutoruka ndege katika anga za Ukraine – ombi ambalo White House imesema litaifanya Marekani kuingia katika mzozo wa moja kwa moja na Russia.

“Hatukubaliani na hoja ya kuwa hilo litakuwa ni hatua muafaka,” msemaji wa White House Jen Psaki alisema (Jumanne). “Kwa sababu marufuku ya kuruka ndege, ambayo aghlabu – watu – wanafupisha kauli hiyo, kwa umuhimu ina maana kuzitungua ndege za Russia na wao kujibu mashambulizi yetu.”

Hotuba ya Zelenskyy inafuatia hotuba mfano wa hiyo aliyoitoa kwa mabunge ya Uingereza, Canada, Umoja wa Ulaya katika wiki za karibuni wakati akiendelea kushinikiza kwa msaada zaidi wa kijeshi na kibinadamu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Mkutano wa NATO

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema wajumbe huko Brussels watakuwa wanajadili yote “madhara ya moja kwa moja ya uvamizi wa Russia” na juhudi za muda mrefu kuimarisha ulinzi wa pamoja wa NATO.

“NATO ina jukumu la kuhakikisha kuwa mzozo huu hauogezeki nje ya Ukraine, na hiyo pia ndio sababu tumeongeza uwepo wetu huko mashariki ya umoja wetu,” Stoltenberg amewaambia waandishi.

Amesema hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ni pamoja na kupeleka “kiwango kikubwa zaidi cha majeshi” katika eneo la mashariki, pamoja na kuongeza majeshi ya majini na angani, mifumo ya makombora ya kujihami na kuwepo mazoezi makubwa zaidi ya mara kwa mara ya kijeshi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin aligusia msaada kwa uwezo wa Ukraine kujilinda wenyewe na vilevile ahadi ya Marekani kumsaidia mshirika yoyote wa NATO atakaye shambuliwa.

“Nafikiri uwepo wetu hapa unapeleka ujumbe kwa ulimwengu kuwa tungali tumeungana katika kuisaidia Ukraine, na tunalaani uvamizi usiokuwa wa haki na bila ya uchokozi dhidi ya Ukraine.

Russia imekataa uwepo wa NATO karibu na mipaka yake na inatakaa kuhakikishiwa kuwa Ukraine kamwe haitajiunga na ushirika huo. NATO inasisitiza nchi zinahiari ya kufanya uamuzi wao juu ya ushirikiano wa kiusalama.

XS
SM
MD
LG