Umoja wa Mataifa unasema takribani raia milioni tatu wa Ukraine wameondoka nchini mwao tangu uvamizi wa Russia takribani mwezi mmoja uliopita katika mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tangu vita vya pili vya Dunia.
Wengi wao walikimbilia nchi jirani lakini idadi inaongezeka huku wengi wanaelekea magharibi.
Treni kutoka Stuttgart inaingia kwenye kituo cha treni cha Gare de I’Est kaskazini mwa Paris, mojawapo ya treni kadhaa zinazowasili kila siku zikiwa na wimbi jipya la wakimbizi wa Ukraine.
Anastasia Starozhitka na mama yake, Maria wanazungumza na wafanyakazi wa chama cha Msalaba Mwekundu ambao wanasalimiana na wakimbizi wapya wanaowasili. Wanawake hao wawili wamefanikiwa kufanya safari ndefu kutoka nchini kwao.
“Tulitokea Kyiv na siku ambayo mnara wa TV uliposhambuliwa, tulikwenda Lviv. Tumekaa wiki moja huko Lviv kwa marafiki zetu kwa usalama, na kisha tulikwenda Berlin hadi paris. Ni hadithi ya kushangaza kwa hakika, kusafiri kuzunguka Ulaya yote kwa sababu ya mtu mmoja wa ajabu dhidi ya dunia,” anasema Starozhitka.
Mtu huyo anayemtaja ni rais wa Rusia Vladimir Putin ambaye majeshi yake yalishambulia mnara wa TV wa Kyiv wiki mbili zilizopita. Uvamizi wake umezua mzozo mkubwa wa kibinadamu.
Starozhitka na mama yake wote ni wakurugenzi wa filamu. Filamu yao inayoitwa “The War OF Chimeras” ilionyeshwa kwenye matamasha ya kimataifa. Inahusu mzozo wa mwaka 2014 katika eneo la Donbas huko mashariki mwa Ukraine baada ya watu wanaotaka kujitenga wanaounga mkono Russia walipojitangazia uhuru. Ilisaidia kuweka misingi ya mapigano ya hii leo.
“Tulienda vitani huko Donbas mwaka 2014 na hii ni kama hadithi yangu ya kibinafsi wakati mpenzi wangu anaenda kwenye vita, na mimi nilimfuata,” Strazozhtika anasema.
Hivi sasa rafiki yake anapigana tena na wa-Russia. Baba na babu yake walipata makaazi ya muda katika mji wa magharibi wa Lviv, ambapo wanaume walio katika umri wa kupigana hawawezi kuondoka nchini humo. Yeye na mama yake ni wakimbizi.
Tuko hapa kuwakaribisha. Kuwaambia kwamba ni sawa, wako salama na kuwaelekeza, kutegemea kile wanachopanga baada ya hapo, anasema Esteve.
Elodie Esteve anafanya kazi na French Red Cross. Shirika lake linafanya kazi na taasisi ya Paris na maafisa wengine wa jiji kuwasaidia watu wa Ukraine kupata makaazi ya muda, msaada wa matibabu na huduma nyingine. Reli ya SNCF ya Ufaransa, kama ilivyo zingine huko ulaya zinatoa usafiri wa bure kwa wakimbizi.
Maelfu yaw a-Ukraine wamepata hifadhi nchini Ufaransa lakini idadi yao inaongezeka haraka. Serikali ya Ufaransa inasema iko tayari kuchukua hadi watu laki moja.
Tofauti na mzozo wa wakimbizi wa mwaka 2015 wa Wa-Afrika, wa-Syria na watu wengine ambao ulileta mwitikio wa majibu mchanganyiko kwa ulaya, wazungu wengi hii leo wanawakaribisha watu wa Ukraine. Viva ni raia wa Paris kutoka Lithuania, yupo Gare de I’Est, kuona kama anaweza kusaidia.
Mshiriki mwingine wa Paris ni Natalia Palubniak, anajitolea kama mkalimani wa Msalaba Mwekundu au red Cross. Yeye anatoka katika mji mdogo magharibi mwa Ukraine.
Anastazia na Maria Starozhitska, wakurugenzi wawili wa filamu raia wa Ukraine wanakaa mjini Paris kwa sasa.
Binti wa Anastazia ana Imani kwamba watarejea Ukraine siku moja.
Tunawasubiri nyumbani ,wanasema, ni jokofu au friji lililojaa chakula, bila kusahau kuitaja familia yako yote iliyobakia.