Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:10

WHO : Afrika iko katikati ya wimbi kamili la tatu la COVID-19


Ramani ya Afrika
Ramani ya Afrika

Afrika iko katikati ya wimbi kamili la tatu la COVID-19 na kuna haja ya kupata chanjo zaidi, Shirika la Afya duniani, WHO, limesema.

Kwa jumla, maambukizi yote, yamevuka alama ya milioni tano, na chanjo zimekwisha, katika angalau nchi saba, za Afrika.

Mkurugenzi wa WHO, Kanda ya Afrika, Matshi-diso Moeti amesema bara hilo linahitaji mamilioni zaidi ya dozi za chanjo, na kwa dharura.

Afrika Kusini, Morocco, Tunisia, Ethiopia na Misri, zimeripoti visa vingi zaidi vya maambukizi barani humo.

Uganda na Namibia zinakabiliwa na wimbi la tatu la virusi hivyo hatari huku idadi ya vifo ikiongezeka kila siku.

WHO inasema Jumla ya watu 136,030 wamefariki kutokana na Covid-19 katika nchi mbalimbali za Afrika.

Aina mpya ya virusi viitwavyo Delta vilivyogunduliwa nchini India viko katika nchi 14 za Kiafrika huku vile vya Beta vilivyogunduliwa nchini Afrika Kusini, viko katika nchi 25.

WHO inasema ingawa hakuna ratiba ya wazi inayoonyesha ni lini chanjo zaidi zitapatikana kuna haja ya dharura ya kuzipata.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG