Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:24

White House: Huenda Iran inashirikiana na Russia kuwadhibiti waandamanaji


Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Karine Jean-Pierre
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Karine Jean-Pierre

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre amesisitiza Jumatano kwamba utawala  wa Biden unawaunga mkono wananchi wa Iran, na kusema inawezekana kuna ushirikiano kati ya Iran na Russia katika kukabiliana na waandamanaji wa Iran.

“Tunasimama na raia shupavu na wanawake jasiri wa Iran ambao hivi sasa wanaandamana kutafuta haki zao za msingi,” Jean-Pierre aliwaambia waandishi wa habari.

Amesema Marekani “ina wasi wasi kwamba Moscow huenda inawashauri Tehran katika hatua bora za kuwadhibiti waandamanaji, wakichukua uzoefu wa Russia wa muda mrefu wa kuzima maandamano ya wazi.”

Jean-Pierre ameongeza kwamba ushahidi kuwa Iran inaisaidia Russia katika vita huko Ukraine “uko wazi na hadharani.”

Ukraine na washirika wake wa Magharibi, ikiwemo Marekani, wamesema droni zilizotumika na jeshi la Russia kuishambulia Ukraine katika wiki za karibuni zilitolewa na Iran. Russia imekanusha kutumia droni za Iran na Iran imekana kuipa Russia droni.

FILE PHOTO: Kiongozi wa kidini wa Iran akiwa amesimama karibu na droni wakati wa mazoezi ya kijeshi katika eneo lisilojulikana nchini Iran.
FILE PHOTO: Kiongozi wa kidini wa Iran akiwa amesimama karibu na droni wakati wa mazoezi ya kijeshi katika eneo lisilojulikana nchini Iran.

“Iran na Russia zimeendelea kuwa karibu zaidi kadiri nchi hizo zinavyozidi kutengwa,” Jean-Pierre alisema. “Ujumbe wetu kwa Iran ni wa wazi kabisa: Acheni kuwaua watu wenu na kupeleka silaha Russia kuwauwa Waukraine.”

Katika mkutano huo na wanahabari naye msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa John Kirby alisema Russia na Iran wanashirikiana kukiuka haki za binadamu na kiraia za Wairan na kuhatarisha maisha ya wananchi wa Ukraine.

John Kirby
John Kirby

“Marekani inasimama pamoja na Iran – wanawake wa Iran na raia wote wa Iran ambao wanautia moyo ulimwengu kwa ujasiri wao. Sisi tutaendelea kuchukua hatua kuhakikisha wale wanaofanya uhalifu dhidi ya waandamanaji wanaokusanyika kwa amani au wanatafuta njia ya kukandamiza haki zao hasa za msingi.”

XS
SM
MD
LG