Mapema mwaka huu, raia wa New Zealand Topher Richwhite, mtoto wa mmoja wa matajiri wakubwa nchini New Zealand, na mkewe Bridget Thackwray, waliitembelea Iran wakikaidi ushauri rasmi kutoka serikali huko Wellington.
Serikali iliwasihi raia wake kutokwenda Iran, ambapo kifo cha Mahsa Amini kilichochea maandamano na ghasia za kiraia.
Msichana huyo wa miaka 22 alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa na polisi wa maadili kwa madai ya kupuuza kanuni kali za kufunika kichwa.
Maafisa wa New Zealand wamesema safari ya Richwhite na Thackwray nchini Iran ilikuwa imesitishwa na mamlaka za Iran na wameruhusiwa tu kuondoka nchini kwa msaada wa serikali ya Wellington.
Maafisa wa serikali wanasisitiza hakuna makubaliano yoyote yaliyofanyika kuwaruhusu wawili hao kuondoka.
Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand Nanaia Mahuta aliiambia radio ya New Zealand katika kipindi cha Checkpoint kuwa mazungumzo na Iran yalikuwa magumu na yenye hisia kali.