Ghasia zilipamba moto nchini Iran tangu kifo cha Amini tarehe 16 Septemba, ambaye alifariki siku tatu baada ya kukamatwa na polisi wa maadili kwa madai ya kukiuka sheria kali ya Jamuhuri hiyo ya Kiislamu kuhusu kuvaa hijabu.
Darzeni ya watu, wengi wao wakiwa waandamanaji, lakini pia maafisa wa usalama, waliuawa wakati wa ghasia hizo. Mamia zaidi, wakiwemo wanawake, walikamatwa.
Tarehe 17 Oktoba, Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya polisi ya maadili pamoja na maafisa 11 akiwemo waziri wa mawasiliano wa Iran, ikiwatuhumu kwa kuhusika katika ukandamizaji wa waandamanaji.
Kama jibu, wizara ya mambo ya nje ya Iran imetangaza katika taarifa vikwazo dhidi ya taasisi nane na watu 12 waishio katika Jumuia ya Umoja wa Ulaya “kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi, kuchochea ghasia na vurugu, ghasia na vitendo vya kigaidi” ndani ya Jamuhuri hiyo ya Kiislamu.
Miongoni mwa vyombo vya habari vilivyochukuliwa vikwazo ni radio ya Ufaransa RFI na radio ya Ujerumani Deutsche Welle.