“Imenifanya kujisikia mgonjwa – nasikia kichefuchefu,” alisema Mmrekani Brooke Raboutou akizungumza na Shirika la habari la Associated Press (AP) Ijumaa katika mashindano ya Kombe la Dunia la upandaji milima huko kaskazini mwa Japan.
“Namuunga mkono kwa asilimia 100, nataka kufikiria kuwa ninaweza kuzungumza kwa niaba ya wanariadha wengi,” aliongeza. “Nimewasiliana naye, nikimwambia kama anataka tufanye kitu chochote kusaidia, kumuunga mkono. Najua anapambana na vita ngumu kwa kweli na kufanya kila anachoweza kuwawakilisha wanawake wa nchi yake.”
Raboutou alisema hakupata majibu yoyote kutoka kwake.
Rekabi, 33, alishiriki mashindano ya Jumapili bila ya kuvaa hijabu, huko Seoul wakati wa fainali ya mashindano ya Asia ya kupanda milima ya Shirikisho la Kimataifa la Michezo. Mara moja alifurahiwa na wale waliokuwa wanaunga mkono wiki kadhaa za maandamano nchini mwake juu ya suala la hijab ambapo kelele zimeongezeka zikiutaka utawala wa kidini nchini humo upinduliwe.
Alirejea Iran nchini kwake na kupokelewa na kundi la waandamanaji waliomshangilia wakiwemo wanawake wakiwa wamevua hijab ambayo ni lazima kuvaa. Katika mahojiano yasiyokuwa na hisia kabla ya kuondoka uwanja wa ndege, aliiambia televisheni ya taifa kuwa kushiriki kwake katika mashindano bila ya kufunika nywele zake ilikuwa “sio kwa makusudi.”
Michezo nchini Iran, kuanzia mashindano ya ligi ya mpira hadi ya kupanda milima, inafanyika chini ya usimamizi wa taasisi zenye mafungamano na serikali. Wanariadha wa kike wanaoshindana nchini na nje ya nchi, iwapo wanacheza mpira wa mkono au kukimbia, wanatarajiwa kufunika nywele zao kama ni ishara ya uchamungu. Iran imefanya kufunika kichwa ni lazima kwa mwanamke, kama ilivyo kwa Afghanistan iliyoko chini ya udhibiti wa Taliban.
Kitendo cha Rekabi ambacho kinaonekana kuwa ni kukaidi amri kimeelezewa kuwa ni tukio chachu nchini Iran. Wanaharakati wanasema inapelekea kuunga mkono maandamano dhidi ya serikali yaliyoibuka baada ya kifo cha Mahsa Amini, miaka 22, ambaye alikamatwa na askari wa maadili wa nchi hiyo kwa kile alichokuwa amevaa.
Katika jamii ya wapanda milima iliyoshikamana barabara, yeye amekuwa ni tumaini kwa wanariadha wengi ambao walikuwa hawamjui – au wanamjua juu juu tu.