Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 11:35

Makundi ya haki za binadamu yanataka msako dhidi ya waandamanaji Iran kuchunguzwa


Waandamanaji nchini Iran Okt 2022
Waandamanaji nchini Iran Okt 2022

Zaidi ya mashirika 40 ya kutetea haki za kibinadamu yanataka baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kujadili msako unaoendeshwa na serikali ya Iran dhidi ya waandamanaji.

Taarifa ya mashirika hayo iliyotolewa Jumatatu inaeleza wasiwasi kwamba Jamhuri ya Kiislamu inakandamiza maandamano kote nchini kutokana na kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Mahsa Amini.

Amini alifariki akiwa katika kizuizi cha polisi mjini Tehran.

Alikamatwa kwa kukosa kufunika nywele zake kwa kutumia hijab.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema kwamba ushahidi unaonyesha namna maafisa wa usalama wanavyotumia risasi kwa makusudi na kutumia nyuma kuwapiga waandamanaji na watu ambao hawashiriki na maandamano, wakiwemo w.

Taarifa hiyo inasema kwamba zaidi ya waandamanaji 200 wameuawa katika maandamano hayo, wakiwemo watoto 23. Zaidi ya waandamanaji 1000, wanaharakati, waandishi wa habari na wanafunzi wamekamatwa katika mazingira ya kutatanisha.

Makundi hayo, yakiwemo Amnesty International na Human Rights Watch, yanataka baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuunda kamati huru kuchunguza ripoti hizo, na kuwawajibisha wahusika.

Wamesema kwamba iwapo jumuiya ya kimataifa itashindwa kuchukua hatua, idadi kubwa ya wanaumme, wanawake na watoto wataendelea kuuawa, kupigwa, kuteswa na kuzuiliwa na polisi.

XS
SM
MD
LG