Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:02

EU yaweka vikwazo kwa makampuni yanayouza ndege kutoka Iran zinazotumiwa na Russia


Makao makuu ya tume ya EU mjini Brussels
Makao makuu ya tume ya EU mjini Brussels

Umoja wa Ulaya Alhamisi umekubaliana kuweka vikwazo vipya kwa makampuni yanayouza ndege zisizokua na rubani (drones) kwa Russia ambazo zinatumiwa kuishambulia Ukraine.

Ofisi ya rais wa Jamhuri ya Czech, mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya hivi sasa imetangaza makubaliano hayo kwenye Twitter leo, ikisema yamefikiwa baada ya siku tatu za mazungumzo na mabalozi wa Umoja wa Ulaya, na vikwazo hivyo vimeanza kutekelezwa kuanzia leo Alhamisi alasiri.

Ofisi hiyo imesema EU itazuia mali za watu watatu na kampuni moja wanaohusika katika uuzaji wa ndege hizo.

Wanajeshi wa Russia wameongeza mashambulizi ya anga tangu wiki iliyopita, huku maafisa wa Ukraine wakieleza kuwa Russia inatumia ndege hizo (drones) zilizotengenezwa na Iran, ambazo hulipuka baada ya shambulio.

Lakini Iran imekanusha kutoa ndege hizo kwa Russia, na Moscow imekanusha pia kutumia drones hizo nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG