Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:58

Iran yapinga vikwazo vya Uingereza


Iran imeshutumu uamuzi wa Uingereza kuweka vikwazo kwa idara yake ya polisi wa kusimamia mila na desturi.

Vikwazo hivyo viliwekwa baada ya kifo cha Mahsa Amini aliyekuwa chini ya ulinzi wa idara hiyo ambacho kimezua mandamano kote katika taifa hilo jamuhuri ya kislamu.

Katika maandamano mabaya yaliyozuka toka Septemba 16 siku kadhaa baada ya kukamatwa binti wa miaka 22 na polisi wa usimamizi wa mila na desturi mjini Tehran kwa kushutumiwa kukiuka kanuni kali ya mavazi ya Iran kwa wanawake.

Katika taarifa yake ya Jumatatu, Uingereza imesema inaweka vikwazo kwa idara hiyo nzima ya polisi, kamanda wa polisi na mkuu wa wanamgambo wa Basij kutoka kikosi cha kimandinduzi cha kislamu.

Katika kujibu hilo, Iran imesema imemtumia barua balozi wa Uingereza aliyepo Tehran siku hiyohiyo, na kumtaka aelezee sababu ya vikwazo hivyo vipya vilivyowekwa.

Imemuelezea balozi juu ya pingamizi kali ya Tehran kwa London kwa kuingilia masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kislamu ya Iran, taarifa hiyo imesema.

Iran inasema dazeni ya watu wameuwawa katika maandamano yaliyo tokana na kifo cha Amini, ikijumuisha wana usalama 18 na mamia ya watu wamekamatwa kwa kile kilichoitwa kufanya mgomo.

XS
SM
MD
LG