Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:35

Israel kutoa taarifa za kijasusi kuhusu ndege za kivita za Iran zinazotumiwa nchini Ukraine


Rais wa Israel Isaac Herzog akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken mjini Washington, Oktoba 25, 2022. Picha ya Reuters
Rais wa Israel Isaac Herzog akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken mjini Washington, Oktoba 25, 2022. Picha ya Reuters

Rais wa Israel Isaac Herzog anapanga kutoa taarifa za kijasusi kuhusu ndege zisizo na rubani za Iran (drones) zinazotumiwa nchini Ukraine na jeshi la Russia atakapokutana leo Jumatano na Rais wa Marekani Joe Biden.

Ofisi ya Herzog imesema Israel inazo picha zinazoonyesha zinavyofanana drones hizo zilizodunguliwa nchini Ukraine na zile za Iran zilizofanyiwa majaribio mwaka 2021.

Ukraine na washirika wake wa Magharibi walisema kwamba matumizi ya hivi karibuni ya drones kuishambulia miji ya Ukraine, ukiwemo mji mkuu Kyiv, yanahusisha drones 136 zilizotengenezwa nchini Iran.

Iran ilikanusha kutoa ndege hizo kwa Russia, na Russia ilikanusha pia kutumia ndege hizo katika mashambulizi yake nchini Ukraine.

Jumanne, Biden alitoa onyo kali kwa Russia dhidi ya matumizi ya bomu chafu au silaha zozote za nyuklia katika vita vyake nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG