Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:43

Waziri Blinken afanya mazungumzo na Papa Francis


Papa Francis akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, mjini Vatican Juni 28, 2021. Vatican Media/­Handout
Papa Francis akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, mjini Vatican Juni 28, 2021. Vatican Media/­Handout

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametembelea Vatican Jumatatu na kukutana na Papa Francis na maafisa wengine.

Blinken na Papa pamoja na mambo mengine wamejadili mabadiliko ya hali ya hewa, haki za binadamu na usafirishaji haramu wa binadamu.

Ziara hiyo inafanyika kabla ya mkutano unaotarajiwa Oktoba kati ya Papa na Rais wa Marekani, Joe Biden, ambaye ni Mkatoliki wa pili kuongoza Marekani.

Mbali na mikutano na Kardinali Pietro Parolin na Askofu Mkuu Paul Gallagher, mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani alipatiwa ziara ya eneo la Sala Regia na Sistine Chapel.

Leo Jumatatu pia, Blinken na Waziri wa Mambo ya nje wa Italia Luigi Di Maio wanasimamia mkutano wa Umoja wa kimataifa wa kukishinda kikundi cha ISIS.

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje walisema mawaziri watajadili juu ya kuendelea na shinikizo dhidi ya kundi hilo la wanamgambo nchini Iraq na Syria, huku pia wakifanya kazi kukabiliana na washirika wa kundi hilo kwingineko ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG