Hata hivyo hakutaja maradhi yake wakati akitoa hotuba yake kama ilivyo kawaida akiomba amani duniani.
Papa Francis hakuweza kuhudhuria ibada jana Alhamisi na pia Ijumaa asubuhi kwa sababu ya maradhi ambayo yanamsababishia maumivu chini ya mgongo na miguu.
Ilielezwa kuwa ni mara ya kwanza tangu achukue wadhifa huo wa juu wa dini mwaka 2013 kwamba Francis ambaye amefikisha miaka 84 mwezi uliopita, amekosa kuongoza tukio muhimu linalofanywa na papa kwa sababu za kiafya.