Maadhimisho ya siku kuu ya krisimasi yanaendelea kote duniani katika mazingira hatarishi kutokana na janga la virusi vya Corona.
Mamilioni ya watu wameepuka kukusanyika kwa wingi kwa sherehe hizo ili kudhibithi maambukizi.
Watu wengi wanaadhimisha krisimasi wakiomboleza baada ya kufiwa na jamaa wao.
Zaidi ya watu milioni 1.7 wamefariki dunia kutokana na virusi vya corona.
Kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis, amehutubia kundi dogo la watu katika misa ya krisimasi, katika kanisa la mtakatifu Petro, nchini Italy.
Waliohudhuria misa hiyo walifuata maagizo ya maafisa wa afya, ikiwemo kuvaa barakoa.