Waungaji mkono wa sheria hiyo wakivaa nguo za kijani wamekuwa wakisherekea mjini Buenos Aires tangu jana usiku.
Baadhi ya waliojitokeza kusheherekea kupitishwa kwa sheria hiyo walionekana wakitokwa na machozi.
Rais wa Seneti Cristina Kirchner alithibitisha uamuzi huo baada ya zaidi ya saa 12 za majadiliano.
Maelfu ya wanawake hutoa mimba kila mwaka katika taifa hilo ambapo karibu watu 3,000 hufariki kwa kutumia njia za kienyeji na haramu amesema rais Alberto Fernandez aliyependekeza mswada huo mapema mwaka huu.
Hii ina maana utoaji mimba unaruhusiwa katika taifa anakotoka Papa Francis hadi wiki ya 14 ya ujauzito.
Hadi hivi sasa ni Uruguay, Cuba na Guyana ndio ambazo zinazoruhusu utoaji mimba kwa hiyari huko Kusini mwa Amerika.