Sheria hiyo mpya kwa jina la kilatino, SPIRITUS DOMINI au Roho ya Mungu inaruhusu wanawake kuhudumu kanisani kwa kusaidia makasisi. Hatua hiyo inaendana na ahadi aliotoa awali ya kufanya marekebisho kwenye kanisa katoliki ambalo kihistoria limekuwa likihudumiwa na wanaume.
Sheria hiyo inasemekana kuwa itaimarisha zaidi msingi wa kanisa pamoja na kuhusisha kila mmoja kwenye shuguli za uinjilisti ingawa papa Francis amesema kuwa jukumu la kuhubiri bado litabaki kwa wanaume.
Kulingana na sheria za kanisa hilo, wanawake hawawezi kuwa makasisi ingawa mwaka wa 2020 papa Francis alibuni tume ya kuchunguza iwapo wanawake wapewe nafasi ya kuhudumu kama makasisi katika siku za mbele.
Iwapo hilo litafanyika basi wanawake watapewa nafasi ya kuhubiri na kubatiza lakini siyo kuongoza misa.